Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya Uorodheshwaji wa Hisa za Benki ya Biashara ya DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).Hii inatokana na kukamilika kwa zoezi la uuzwaji wa hisa hizo kwa umma na kwa wanahisa lililokamilika hivi karibuni kwa ufanisi. Wengine kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka, Meya wa Dar es Salaam , Isaya Mwita, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya Uorodheshwaji wa Hisa za Benki ya Biashara ya DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hii inatokana na kukamilika kwa zoezi la uuzwaji wa hisa hizo kwa umma na kwa wanahisa lililokamilika hivi karibuni kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka, akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya Uorodheshwaji wa Hisa za Benki ya Biashara ya DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hii inatokana na kukamilika kwa zoezi la uuzwaji wa hisa hizo kwa umma na kwa wanahisa lililokamilika hivi karibuni kwa ufanisi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama akizungumza katika hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza katika hafla hiyo
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akigonga kengele kuashiria tukio la Uorodheshwaji wa Hisa za Benki ya Biashara ya DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia) akishikana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka wakati wa hafla ya Uorodheshwaji wa Hisa za Benki hiyo katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE). Katikati ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (wa pili kulia), Meya wa Ubungo, Boniface Jacob (kushoto), na Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka wakifurahi wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu kijaji (kulia), akizungumza nao baada ya kukamilika kwa tukio la uorodheshwaji wa hisa za DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jijini humo leo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (Wanne kushoto), akipiga picha ya pamoja na maofisa wa DSE, DCB na wageni wengine waalikwa mara baada ya kukamilika kwa hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (katikati), akipiga picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (kutoka kushoto), Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa mara baada ya kukamilika kwa tukio la Uorodheshwaji wa hisa za Benki ya Biashara ya DCB katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).
…………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, ameipongeza benki ya biashara DCB kwa kufanikisha zoezi la uuzaji wa hisa zake kwa ufanisi mkubwa.
Pongezi hizo amezitoa jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya uorodheshwaji wa hisa za DCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
“Wizara ya fedha na mipango inajivunia mafanikio ya Benki ya Biashara ya DCB, ambayo wamiliki wake wakubwa ni Halmashauri zetu hususani Manipaa ya Dar es Salaam pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam” alisema Mheshimiwa Naibu waziri.
Alisema anafarijika kuona mshikamano uliopo kati ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, DSE, Benki Kuu ya Tanzania, Kampuni ya Ushauri katika Masoko ya Mitaji na Dhamana na mawakala wa uuzaji wa Hisa katika kuisaidia benki kufanikisha malengo yake ya kuongeza mtaji kwa kuuza hisa zake kwa umma.
“Uuzaji wa hisa kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam, ndio njia sahihi ya kuongeza mtaji, na pia kuwamilikisha wananchi wa kawaida uchumi wa Taifa lao”
Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa serikali inajivunia uwekezaji wa Benki ya biashara ya DCB kwa kuwa ni uwekezaji wa ndani, na uwekezaji huu umewezekana kwa sababu serikali imetimiza kwa vitendo wajibu na adhima yake ya kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wadau wake.
Pamoja na hayo alisema DCB imefanikiwa kuuza hisa milioni 36.6, ikiwa ni zaidi ya malengo ya awali ya kuuza hisa milioni 33.9, hadi kukamilika kwa zoezi la uuzaji hisa benki imefanikiwa kukusanya sh. Bilioni 9.7 sawa na asilimia 108.99 ya matarajio ya awali ya kukusanya shilingi Bilioni 8.9.
“Mauzo haya ya hisa yamefanyika kwa bei ya punguzo ya shilingi 265, badala ya bei ya soko ya shilingi 340 kwa hisa, sambamba na mafanikio haya, DCB imetangaza gawio la shilingi bilioni 1.6 kwa wanahisa wake katika mwaka 2018 na hivyo kufuta hasara ya shilingi bilini 6.0 iliyoripotiwa mwaka 2019,” aliongeza Naibu Waziri Ashatu.
Akimkaribisha Mheshimiwa Naibu Waziri, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka alisema mafanikio katika mauzo ya hisa zao inadhihirisha imani waliyonayo wawekezaji wa benki ya DCB na masoko ya mitaji hapa nchini. Na kwa kupitia mauzo hayo mtaji wa DCB unatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi bilioni 16.9 hadi kufikia shilingi bilioni 26.7 ikiwa ni ongezeko la asilimia 57.
“Lengo letu katika uongezaji mtaji ni kuhakikisha kuwa benki ina uwezo wa kuleta ushindani, sambamba na kuchochea ukuaji wa mageuzi makubwa ya kibenki yatakayoifanya benki iimarike zaidi,” alisema mwenyekiti wa bodi.
Naye Mkkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Godfrey Ndalahwa katika hafla hiyo alisema kupitia mpango mkakati wa mwaka 2018 na jitihada za wadau mbalimbali wa benki ya DCB, kwa mwaka wa fedha mwaka 2018 imefanikiwa kupata faida ghafi ya shilingi bilioni 1.6, ikilinganshwa na hasara ya shilingi bilioni 6.9 kwa mwaka 2017.
“Benki inaendelea na mipango ya serikali ya kuhakikisha wajasiriamali wadogo wadogo wanapata fursa, wanapata ufumbuzi wa kifedha wenye manufaa na wa gharama nafuu ambao hutimza mahitahi yao kulingana na mpango wa kimkakati wa benki.
“Benki itaendelea kujikita na uuzaji kwa bidhaa za mikopo ya nyumba na mikopo midogo midogo huku ikichagua soko la wajasiriamali wadogo, ikumbukwe lengo kuu la kuunzishwa benki ilikuwa kusaidia wajasiliamali wadogo kwa kutoa mikopo ya masharti nafuu…. napenda kutoa rai kwa halmashauri zote nchini kuwekeza katika benki yetu na kufanya biashara na benki ikiwemo kufungua akaunti za makusanyo ya mapato. Benki yetu ni chanzo kizuri cha uwekezaji ” aliongeza mkurugenzi huyo.
Aidha Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ua Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama alisema mafanikio ya yaliyotokana katika zoezi la uuzwaji hisa za Benki ya DCB, ni uthibitisho kwamba wapo watanzania wengi wanopenda kushiriki katika mfumo rasmi wa kifedha kwa kuwekeza katika masoko ya mitaji hivyo jitihada zaizi zinahitajika kuongeza bidhaa nyingi na uwekezaji katika masoko ya mitaji hapa nchini.
Zoezi la uuzaji wa Hisa za DCB lilizinduliwa Novemba 12 2018 nna kuhitimishwa Januari 31, 2019 ambapo hisa 36,635,435 ziliuzwa ikivuka kiwango cha hisa 33,913,948 zilizopangwa awali.