NA EMMANUEL MBATILO
Wazazi, walezi pamoja na Wadau Mbalimbali wameombwa kuhakikisha wanaweka juhudi za kusaidia kutokomeza mimba za utotoni na ukeketaji unaendelea siku hadi siku na kurudisha nyuma maendeleo ya Maendeleo ya Mtoto Wa like kiuchumi
Wito huo umetolewa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Wa Shirika lisilo la kiserikali linalopinga suala zima za ndoa za utotoni na ukeketaji Plan international, Ndg. Oywnneth Wong katika maadhimisho ya maadhimisho ya siku ya Familia Duniani amesema jinsia ya kike wamekuwa ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo kwani husababishwa na mila potofu,na ukosefu wa uelewa katika Jamii.
Hata hivyo kwa upande wake Mkuu Wa idara ya Afya ya Uzazi katika shirika la Plan international, Dkt. Katanta Semwanza amesema msichana anayeolewa chini ya umri Wa miaka kumi na nane bado hajakomaa kiakili kwani wengine hukutana na changamoto mbalimbali wanapoenda kujifungua ikiwemo vifo pamoja na kutoka damu nyingi.
Naye mwandishi Wa kitabu cha Mabala the farmer Richard Mabala amesema licha ya Juhudi mbalimbali zinazofanyika lakini tatizo ni sungu kutokana mfumo dume uliopo katika baadhi ya jamii,na mazingira wezeshi ya watoto wa kike kujikomboa bado ni changamoto mfano mashuleni hakuna mabweni,vifaa vya kutosha vya kufundishia hivyo kuwakatisha tamaa kuendelea na masomo.
Kwa upande wake afisa uhusiano wa plan international Bi. Jesca Slaa ameiomba serikali kusaidia kutokomeza tatizo hilo linalowakumba Watoto wa kike kwani wengine wamekata tamaa na maisha kutoka na vikwazo wanavyopitia kutoka na mifumo dume ilipo katika jamii zao.