Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali inapotwaa maeneo ya wananchi kwa ajili ya matumizi ya Jeshi ikiwemo kuwalipa fidia wananchi hao, ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 15, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akieleza mikakati ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wa mikoa mbalimbali ikiwemo Mtwara, Lindi na Dar es Salaam wanaunganishiwa huduma ya gesi majumbani ili kuchochea maendeleo .
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Dkt Angelina Mabula akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira mhe. Mussa Sima leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati mhe. Subira Mgalu akisisitiza wakandarasi wote kutekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini (REA) kwa wakati ili kutimiza azma ya Serikali kufikisha umeme kwa wananchi wote Vijijini.
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 15, 2019. Katikati ni Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 15, 2019.