Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James (kulia) akiwa amemshika mkono na kuzungumza jambo na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za elimu za juu Tanzania (TAHLISO) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wanafunzi vyuo vya elimu ya Juu nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki Frank Nkinda (kushoto) baada ya kumalizika kikao ambacho kimefanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo jijini Dar es salaam
…………………………..
NA MUSSA KHALID
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam imewataka Askari wa SUMAJKT wanaolinda Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuhakikisha wanakuwa na ueledi,na kuheshimu utu wa kazi ili kuondokana na changamoto baina yao na wanafunzi wa Chuo hicho.
Hayo yamejiri kufuatia kusambaa kwenye mitandao ya kijamii picha za matukio mawili tofauti likiwemo la mwanafunzi aliyezuiliwa kuingia chuo kwa kutokuwa na kitambulisha hali iliyosababisha mvutano na askari na tukio jingine ni mwanamama muhudumu wa chakula chuoni hapo ambapo alikwenda chuoni akiwa na mavazi ambayo yanazuiliwa chuoni hapo.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amekemea kitendo cha namna Askari hao wamepambana na wananchi kwa kutumia nguvu kubwa hali ambayo sio sawa.
Amesema mambo ambayo wamebaini ni kwamba matukio hayo yamefanyika ambapo lakwanza ni lilikuwa ni la mwanafunzi ambaye alizuiliwa kuingia chuo kwa kutokuwa na kitambulisho ambao ni utaratibu wa chuo hicho hivyo kusababisha mvutano baina ya Askari na mwanafunzi huyo na la pili
‘Kamati ya usalama ya Wilaya iliona kwamba upo umuhimu wa kuja kujiridhisha ya kuwa nini kilitokea,kwa nini kilitokea nani alifanya na ni hatua gani zimechukuliwa kwa sababu huo hi wajibu wetu kama serikali kulinda taratibu zilizowekwa hasa kikatiba’amesema DC James
Aidha licha ya SUMAJKT kuchukua hatua dhidi ya askari hao ametoa wito kwa askari kutotumia nguvu kupambana na wanafunzi katika taasisi yeyeto huku akieleza kuwa pia wamebaini changamoto ya wanafunzi kupata shida wakati wakiingia chuoni kwa sababu ya muongozo wa mavasi ikiwa ni pamoja kutokuvaa soksi.
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za elimu za juu Tanzania (TAHLISO) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wanafunzi vyuo vya elimu ya Juu nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki Frank Nkinda amekipongeza Chuo cha NIT kwa kuchukua hatua kwa tukio hilo huku Rais wa Serikali ya wanafunzi NIT Jeremia Stephen ameleza kuwa tangu kutokea tukio hilo ulinzi wa wanafunzi umimarika.
Hata hivyo Jumuiya hiyo imesema itaendelea kuwa karibu na wanafunzi wot wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuwa wataendelea kushirikiana kuzipata haki zao huku akitoa wito kuwa wahakikishe wanatii sheria kanuni na taratibu ambazo zimewekwa ndanbi ya vyuo.