
Muonekano wa vituo vya ukaguzi wa magari na vyombo vingine vya moto.
Vituo vya ukaguzi wa magari na pikipiki.
KUFUATIA ziara
iliyofanywa nchini Misri na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni imeanza
kuonesha matunda ambapo baadhi ya wawekezaji kadhaa ikiwepo Kampuni ya
Kimataifa ya GS Investment Group yenye makao makuu yake Cairo Egypt nchini humo
kuonesha nia ya kuwekeza katika eneo la mazingira.
Akizungumza kwa njia ya
simu Afisa Mtendaji wa Kampuni hiyo (CEO) Gasser El-Sayed ambaye anaiendesha yenye mapato ya dola za kimarekani billion
mbili (2 billion USD ) kwa mwaka ameonesha nia ya kuwekeza katika eneo la
VEHICLE INSPECTION CENTERS na TRAFFIC Management Solutions kwenye mikoa yote
Tanzania kwa njia ya PPP.
El-Sayed alisema kwa sasa
wameanza kufuatilia vibali, utaratibu na kanuni zote za uwekezaji kutoka
Serikalini kabla ya kuanza Uwekezaji huo nchini.
“Baada ya ziara ya
COP27 ya Rais wa Tanzania Egypt, tumeona ni fursa njema kuleta uwekezaji wetu
Tanzania kama tulivyofanya Ghana, Chad, Nigeria, Dubai na Saudi Arabia, na
tumekusudia kuja kuwekeza kwenye eneo la VEHICLE INSPECTION CENTERS na
tutajikita zaidi katika masuala ya usalama barabarani ambapo tutatumia
mageuzi ya kidigitali katika kufanya shughuli hiyo” alisema.
El-Sayed alisema
mazingira ya mradi huo utaisaidia Serikali kukusanya mapato kwa ajili ya
maendeleo ya nchi kama Ilivyokuwa kwenye nchi nyingine ambapo Mapato
yaliongezeka kwa asilimia 60% baada ya uwekezaji wao.
Alisema katika kutekeleza
suala hilo watajenga mitambo maalumu Nchi Nzima ambazo zitatumika kukagua
magari yote na vyombo vingine vya moto kama pikipiki ambavyo vitakuwa havina
ubora, kama kutoa moshi na uchakavu na kuhakikisha Usalama wa barabarani.
Alisema kampuni hiyo
imekuwa ikifanya kazi nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika na
imekuwa ikijishughulisha kutengeneza mbolea, masuala ya afya, bidhaa za ngozi,
na kwa sasa wana mkataba wa kutengeza Pia Vifaa Vyote vinavyotumika kwenye World
Cup Qatar na FIFA ikiwemo mipira na mambo mengine mbalimbali.
Alisema tayari kampuni
hiyo imekuwa ikifanya majadiliano na Serikali kwa takribani Mwaka na nusu sasa
na wana imani michakato iko kwenye hatua za mwisho kuhusu masuala na maeneo
ambayo serikali itapendekeza kufanya.
Alisisitiza kuwa uwekezaji huo kwa
awamu ya kwanza wataanza na kazi hiyo na baadae iwapo watakubaliwa wataingia
katika masuala mengine ikiwemo kujenga viwanda na mifumo mbalimbali ya kuweza
kusaidia Serikali kwenye ukusanyaji wa mapato.