Tuesday, November 24, 2026

Alex Sonna

Latest updates on ministries, public service, parliament, policy decisions, and national administration.

26397 Stories
WIZARA YA ARDHI YAFUTURISHA WATUMISHI WAKE

WIZARA YA ARDHI YAFUTURISHA WATUMISHI WAKE

Sehemu ya watumishi wa wizara ya ardhi wakipata futari ya pamoja Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati…

KIRIA AZINDUA POLISI JAMII CUP 2023 MIRERANI

KIRIA AZINDUA POLISI JAMII CUP 2023 MIRERANI

Na Mwandishi wetu, Mirerani MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Kiria Ormemey Laizer, amezindua rasmi mashindano ya Polisi Jamii Cup 2023 Mirerani…

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUIWEZESHA TAZARA

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUIWEZESHA TAZARA

  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete (kulia) na Mshauri wa Waziri kutoka Ubalozi wa China Nchini, Suo Peng (kushoto) wakiweka maua katika moja…

PICHA KATIKA MATUKIO WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA

PICHA KATIKA MATUKIO WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, bungeni jijini Dodoma Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akislimiana na Mbunge wa Mbulu…

MRADI WA MAJI MWINDI WAZINDULIWA,KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AWAPONGEZA WAHANDISI WA RUWASA KUTEKELEZA MRADI HUO KWA UBORA

MRADI WA MAJI MWINDI WAZINDULIWA,KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AWAPONGEZA WAHANDISI WA RUWASA KUTEKELEZA MRADI HUO KWA UBORA

  Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mtwara Mhandisi Hamis Mashindike akionyesha mchoro wa mradi wa maji wa Mwindi unaohudumia zaidi ya wakazi 3,465 wa kijiji cha Mwindi na Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara,kulia mkimbiza Mwenge Kitaifa Juma Silima Sheha. Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilayani Mtwara Mhandisi Hamis Mashindike akieleza jambo kwa mkimbiza mwenge wa Uhuru Kitaifa Juma Silima Sheha,kabla ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim kufungua mradi wa maji Mwindi uliotekelezwa na Ruwasa kwa gharama ya Sh,milioni 800,521,075. Mkuu wa wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara Anafi Msabaha,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwindi(hawapo pichani)wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru kufungua mradi mkubwa wa maji kijijini hapo,kulia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Kaim.  Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Kaim, akiondoa kitambaa kufungua  rasmi mradi wa maji Mwindi  kijiji cha  Mwindi Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani  Mtwara,kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mtwara Erica Yegella. Meneja wa Ruwasa mkoa wa Mtwara Mhandisi Prim Damas wa sita mstari wa mbele,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ruwasa wilaya ya Mtwara na mkoa baada ya Mwenge wa Uhuru kufungua mradi wa maji Mwindi unaohudumia vijiji viwili vya Mwindi na Mbawala. Tenki lenye uwezo wa kuchukua lita 100,000 lililojengwa katika mradi wa maji Mwindi wilayani Mtwara ambalo litahudumia  takribani wakazi  1,593 wa kijiji cha Mwindi.  Moja kati ya vituo vya kuchotea maji kilichojengwa katika kijiji cha Mwindi wilayani Mtwara na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa). Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwindi wilayani Mtwara,wafuatilia matukio ya uzinduzi wa mradi wa maji  wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.  Na Muhidin Amri, Mtwara WAKAZI wa kijiji cha Mwindi na Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara,wameondokana na kero ya muda mrefu ya huduma ya maji safi na salama,baada ya wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Mwindi. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim,meneja wa Ruwasa wilayani Mtwara Hamisi Mashindike alisema mradi huo utahudumia zaidi ya wananchi  3,465 kati yao 1,593 wanatoka kijiji cha Mwindi na 1,872 wa kijiji cha Mbawala. Alisema,katika bajeti ya mwaka 2022 serikali kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uvico-19 imeipatia Ruwasa wilaya ya Mtwara jumla ya Sh.milioni 800,521,075 ili kutekeleza mradi huo. Alisema,utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Januari na kukamilika mwezi Machi chini ya usimamizi wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) wilaya ya Mtwara. Alieleza,mradi wa maji Mwindi ulianzishwa kwa lengo la kusogeza na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika umemaliza kabisa changamoto ya huduma hiyo kwa wakazi wa vijiji hivyo. Kwa mujibu wake,mradi umehusisha ujenzi wa mateki mawili yenye ujazo wa lita 100,000 kila moja ambayo yamejengwa katika kijiji  cha Mwindi    ambapo moja ni la juu  ya ardhi na lingine kwenye mnara wa mita 12. Mashindike alitaja kazi nyingine zilizotekelezwa ni ujenzi wa vituo(virula)12 vya kuchotea maji,ufungaji wa pampu mbili na kulaza mabomba ya maji umbali wa mita 14.363. Alibainisha kuwa,kati ya fedha hizo Sh.milioni 302,077,979.00 zimetumika kununua pampu mbili na Sh.milioni 498,443,096.00 zimelipwa kwa mkandarasi ambapo wananchi wa vijiji hivyo wamechangia Sh.milioni 3. Alisema,mradi umezingatia sera ya maji ya kumtua mama ndoo kichwani na umezingatia umbali usiozidi mita 400 kutoka kituo kimoja na kingine,na ameishukuru serikali kutoa fedha zilizofanikisha utekelezaji wa mradi huo. Meneja wa  Ruwasa alisema,mpaka sasa jumla ya kaya 21 na taasisi 7 zimeunganishiwa huduma ya maji majumbani ili kurahisisha uwepo wa maji karibu na kwenye makazi yao. Aliongeza kuwa,kukamilika kwa mradi huo kutasaidia na kuwezesha wananchi hasa vijana na akina mama kuongeza ajira kwani watatumia maji hayo kulima bustani za mboga na hivyo kuinua kipato cha kaya husika na kuimarisha hali ya lishe katika jamii inayozunguka. Pia alisema,mradi huo utawezesha kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kutoka asilimia 56.66 ya mwaka 2022 hadi asilimia 57.6 mwaka 2023,kutatua changamoto ya maji iliyokuwepo katika vijiji hivyo,kupunguza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko katika jamii kwa sababu ya kutumia maji safi na salama na kuchochea maendeleo ya watu na ustawi wake na kutoa ajira za muda mfupi 40 na muda mrefu 1.…