*********************************************
Na: Fadhila Kizigo Kocha Mwandishi 0673854979
Huku uswahilini kwetu tuna msemo unasema usicheze mbali unga robo ni kweli ni kutokana na hali zetu za maisha pengine hivyo kuchangamka mapema ni vizuri zaidi kwani utajihakikishia kupata ridhiki kwa wakati huo .
Yanga hii ipo moto kweli kweli yaani kama gari ndio lishawaka hivyo dereva yuko safarini ni kweli timu ya Yanga imeanza vizuri mpaka sasa wanakaribia kumaliza duru ya kwanza kwenye ligi kwa kucheza michezo kumi na sita bila kupoteza mchezo hata mmoja hadi sasa kibindoni wakiwa na alama 40 wakifuatiwa na wapinzani wao Simba wakiwa na alama 32 na michezo kumi na nne tofauti ni alama nane na Simba wakiwa na faida ya michezo miwili na kama atafunga michezo hio tofauti ni alama mbili tu na Yanga.
Kwa tofauti hio ya alama nane na faida ya michezo miwili huwezi kusema kuwa Yanga ndio mabingwa msimu huu na hii inatokana pia mtu aliyepoteza mchezo anafaida kubwa kwani ameonja radha ya kupoteza mchezo kikubwa ni kuomba kuwa Yanga hata kama watapoteza mchezo wasipotee kwenye msitali mara nyingi inatokea kwa timu ambazo zinapata matokeo wakati wote endapo anapoteza basi hupotea kabisa kwenye mstari na kupelekea kupoteza michezo mingi baada ya kupoteza.
Wanachotakiwa Yanga ni kuendeleza ushindi kwa kupata magoli mengi ili kujihakikishia kusalia kileleni na kwa aina ya wachezaji wa Yanga waliokuwepo na waliosajiliwa kwenye dirisha hili dogo huenda ndio msaada mkubwa wa kupelekea ushindi na kuwaweka kwenye mbio za kuufukuzia ubingwa.
Bingwa anaweza kuwa Simba au Yanga na mwengine yeyote huu sio mda sahihi wa kusema nani ni bingwa ikiwa ndio kwanza moto umewaka kwa kila mmoja anayeshiriki ligi.
Imeandaliwa Na: Fadhila Kizigo Kocha Mwandishi 0673854979 Instragram fadhilakizigo19