Naibu
Waziri wa maji Mhandisi
Marryprisca Mahundi katikati akiingia kwenye feri wilayani Pangani
wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya
Pangani Mwalimu Hassani Nyange kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga
Mhandisi Upendo Lugongo
Naibu
Waziri wa maji Mhandisi
Marryprisca Mahundi akizundua mradi wa Maji wa Kijiji cha Mbulizaga
wilayani Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo kushoto
ni
Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa
mazingira Vijijini RUWASA wilayani Pangani Zuberi Yahaya Naibu Waziri wa maji Mhandisi
Marryprisca Mahundii
Naibu Waziri wa maji Mhandisi
Marryprisca Mahundi kulia akimsikiliza Meneja wa Ruwasa wilaya ya Pangani Zuberi Yahaya na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
Naibu
Waziri wa maji Mhandisi
Marryprisca Mahundi kulia akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa
wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakati wa ziara yake ya siku
moja wilayani humo
Naibu Waziri wa maji Mhandisi
Marryprisca Mahundi amemtaka Meneja wa Wakala wa maji Safi na usafi wa
mazingira Vijijini RUWASA wilayani Pangani Zuberi Yahaya kujitathimini utendajikazi wake
kutokana miradi ya maji kushindwa kutekeleza kulingana na kasi inayotakiwa.
Agizo hilo alilitoa baada ya kukagua
miradi ya maji ya katika kijiji Cha Msaraza na Mkalamo ikiwa ni sehemu ya ziara
yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Pangani
Alimtaka Meneja huyo kujitathimini
kama nafasi hiyo anaiweza kwani miradi imeshindwa kutekelezwa huku wananchi wakiendelea
kuteseka na kero ya ukosefu wa maji Safi na salama.
“Tunapaswa kukuondoa sio ndio
lakini niwaambie wataalamu acheni kufanya kazi kwa mazoea nyie wataalamu siasa
katika ufanyajikazi sio nzuri kwani wananchi wanahitaji maji sio maneno
tuuu” alisema Waziri huyo.
Aliwataka watendaji wa Ruwasa
kuachana na kufanyakazi kimazoea bali wafanyakazi kwa kasi ambayo itaharakisha
maendeleo na wananchi kupata huduma ya maji Safi na salama.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,
Meneja RUWASA wilaya ya Pangani Rajab Yahaya alisema kuwa wakala huo
unatekeleza miradi mitano ya maji katika wilaya hiyo ambalo utakapokamilika
utasaidia kuongeza kiwango cha huduma kutoka asilimia 35%hadi 80%.
Hata hivyo aligusia suala la
kusuasua kwa miradi ya Msaraza na Mkalamo ambapo alisema imechelewa kutokana na
ucheleweshaji wa fedha za miradi hatua ambayo imeshindwa kuendelea kama
ilivyopangwa.
Alisema kuwa Licha ya kuwepo kwa
vifaa lakini fedha za kuwalipa mafundi zilichelewa hali ambayo imesababisha
miradi hiyo kusimama kwani wanapofanya kazi wanapaswa kulipa siku hiyo hiyo.
Hata hivyo kwa upande wake, Meneja
wa Wakala wa maji Safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA mkoani Tanga Mhandisi
Upendo Lugongo alisema kuwa tayari wamelichukua hilo na kuhaidi kulisimamia
kuanzia Jumanne mradi utekelezwe ili uweze kukamilika ifikapo mwezi Machi 2021 mwaka
huu ili wananchi waweze kupata maji.
Mhandisi Upendo alisema awamu ya pili
wameshafanya usanifu Mkalamo na umefika mwisho hivyo watu wa Mkalamo baada ya
awamu ya kwanza kwisha awamu ya pili itakayoanza mwaka 2021/2022 nao wapo
kwenye mpango watapatiwa maji.