Zanzibar
Chama cha AAFP kimesema ili maridhiano yaliofikiwa Zanzibar yalete manufaa kwa jamii vyama vingine vya siasa vishirikishwe kuondosha hofu ni makubaliano kati ya CCM na ACT Wazalendo.
Pia kimedai ni busara nafasi kumi za uteuzi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi tano vikapewa vyama vilivyoshiriki Uchaguzi mkuu.
Hayo yameelezwa na Makamo Mwenyekiti wa AAFP Omar Juma Said aliyesema maridhiano hayo endapo yatabaki kwenye sura ya sass yanaweza kupoteza afya na kutoheshimika.
Omar amesema maridhiano ni jambo jema katika jamii hivyo dhamana hiyo isiwe imebebwa aidha na wanasiasa au vyama viwili.
Amesema kasoro au dosari zinazotokea zanzibar haziachi athari kwa vyama viwilo badala yake yamapozuka majanga huwaumiza wafuasi wa CCM ,ACT wazalendo na wa vyama vingine
Amesema maridhiano yaliofikiwa zanzbar hayapendezeshi. Kuonelana ni ya CCM na ACT Wazalendo na kuviweka kando vyama vingine .
Omar amesema CUF na CCM toka mwaka 1995 kimeshiriki katika muafaka lakini sasa hakishirikishwi jambo ambalo amesema si sahihi.
Amesema huo ni katika udhaifu unaonyesha kubibagua baadhu ya vyama vinavyodhaniwa vidogo wakati hakuna chama kidogo mbele ya sheria.
Omar amesema oinapotumika jina maridhiano ya Zanzibar wakati ni ya vyama viwili kwa niaba ya Zanzibar na watu wake, ameziita hizo ni rafu za kisiasa.
Aidha Makamo Mwenyekiti wa AAFP amestushwa na matamshi ya makamo wankwanza wa Rais Maalim Seif sharif Hamad aliyesisitiza dhamira ya Act wazalendo ya kuendelea na mashitaka yale icc haijafutika.
Amesema Ikiwa kweli vyama hivyo vimefikia maridhoano ya dhati na kweli kuendeleza mashitaka hukobicc ni jambo linalozidisha hofu.