************************************
Makamo wa kwanza wa Rais wa SMZ Maalim Seif Sharif Hamad amesema amejidhatiti kumshauri na kutimiza majukumu yake atakayopangia na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kwa mujibu wa Katiba.
Amesemai ameridhishwa na malengo ya utendaji wa kazi za serikali za kuondosha kadhia za rushwa, ubadhirifu na ukwapuzi wa mali za umma.
Msimamo huo umetolewa na Makamo huyo wa kwanza wa Rais zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad aliyesema atatimiza wajibu wake wa kumshauri Rais ili kushamirisha maendeleo .
Amesema kwakuwa yeye ni makamp wa kwanza Rais SMZ atatekeleza majukumu hayo na mengine atakayopangiwa na Rais .
Amesema hatakaa kimya atakapopoona mambo yakienda shaghalabaghala au kuyatazama bila kuichukua hatua kwa niaba ya Serikali.
Aidha Mwanasiasa huyo mkongwe amesema kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa(SUK) si matakwa ya kisiasa bali ni mahitaji ya kikatiba na kisheria .
Amesema kuwepo kwa serikali hiyo ni maamuzi yaliotokana na rodhaa pia utashi wa wananchi wote wa zanzibar.
Maalim seif amesema serikali haitamvumilia watendaji wavivu, wazembe na wapiga porojo au wenye urasimu badala yake kila mmoja atimize wajibu wake.
Amesema hayo ni matakwa ya Rais yanayomtaka kila mtendaji smz kujituma bila kusimamiwa kwani Rais anavhotaka no uadilfu na uwajibikaji katika uendeshaji wa seriakli yake.
Maalim seif amesema kinachotakiwa ni kulauniwa kiwango cha ufanisi , nidhamu kwa kufuata sheria na motisha utakaoongeza tija na kuleta manufaa.