Kaimu Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani
akihutubia mahafali ya 10 ya Shule ya Sekondari Utaho iliyopo wilaya ya Ikungi,
mkoani Singida jana.
wa kisima hicho ambacho hakijaanza kufanya kazi kutokana na kukosa mabomba ya
kusambazia maji
Wanafunzi wakiingia kwenye viwanja vya shule hiyo kabla ya
kuanza mahafali hayo
Maandamano kuelekea kwenye viwanja kabla ya kuanza kwa
sherehe za mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Utaho, Mwavita
Malagila
Meza kuu ikishiriki kuimba wimbo wa Taifa
wakiimba wimbo wa uzalendo kabla ya mahafali hayo
Wahitimu wakiingia kwenye viwanja vya shule hiyo kabla ya
kuanza mahafali hayo.
Ndahani akikagua moja ya visima vilivyochimbwa kwa umahiri
mkubwa ndani ya shamba la mwekezaji huyo kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa
maji kwa jamii inayozunguka maeneo hayo.
Embe zilizotokana na shamba hilo lililopo eneo la Utaho
wa Bodi ya shule ya sekondari Utaho, Idd Siph, (kushoto) akimwelekeza jambo
mgeni rasmi wa mahafali ya 10 ya shule hiyo Frederick Ndahani (wa pili kulia).
Wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Utaho ‘A’ Shaban Daghau, Mwalimu Mkuu wa
shule ya msingi Utaho, Yasini Juma, Mwenyekiti wa Kijiji cha Utaho ‘B’ Omari
Chima, na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Samamba iliyojengwa kwa nguvu ya
wananchi, Japhet Pwiti.
Sherehe za mahafali hayo zikiendelea.
Ndahani akikagua shamba bora la zao la embe ambalo limelimwa
kwa tija kubwa na kuonyesha matokeo makubwa ndani ya muda mfupi, kulia ni
mwekezaji mzawa wa shamba hilo, Aqlan Gharib maarufu Turu Best, eneo la Utaho,
Ikungi, Singida
Mwonekano wa shamba hilo ambalo kama litatumika kama shamba
darasa kwa makundi rika mbalimbali ndani ya jamii litainua tija ya kilimo ndani
ya mkoa wa Singida.
WITO umetolewa kwa wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika kuwapa uangalizi wa karibu vijana wanaomaliza kidato cha nne ili kuwanusuru kutumbukia kwenye majanga yanayoweza kuhatarisha mustakabali mzuri wa ndoto zao.
Akihutubia sherehe za mahafali ya 10 ya Shule ya Sekondari Utaho, iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani hapa jana, Kaimu Afisa Vijana mkoa wa Singida, Frederick Ndahani, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Dkt Rehema Nchimbi, alisema ni jukumu la mzazi kupokea kijiti kile kile cha mwendelezo wa maadili mema kutoka kwa walimu wao, pindi vijana wawapo majumbani.
“Wazazi msiwe mbali na vijana hawa, tushirikiane kuhakikisha kile walichojifunza shuleni hata wakiwa nyumbani wanaendelea kukiishi katika misingi ya uzalendo,” alisema Ndahani.
Alisema mustakabali chanya wa maendeleo ya Tanzania katika muktadha wa ustawi wa kiuchumi, amani na usalama wa nchi upo mikononi mwa vijana hao, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwatupia jicho la karibu katika kipindi hiki wanapoandaliwa kimasomo.
Pamoja na mambo mengine, aliwasisitiza wazazi katika kipindi hiki kuwa makini dhidi ya genge baya la wasafirishaji haramu wa binadamu wanaopita-pita kuwarubuni vijana, hususani watoto wa kike mkoani hapa kwa kigezo cha kwenda kuwatafutia ajira zenye maslahi makubwa jambo ambalo sio la kweli.
“Katika hili wazazi tuchukue tahadhari kubwa…hali siyo ya kuridhisha kutokana na mabinti wengi kuendelea kusafirishwa nje ya nchi kwa siri, kwa ahadi za kutafutiwa ajira zenye mshahara mnono jambo ambalo sio kweli, na kinyume chake hugeuzwa watumwa kwa kufanyishwa biashara za ngono na madawa ya kulevya kwa maslahi ya waliowasafirisha” alisema Ndahani.
Aidha, akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa Nchimbi kwa vijana hao, Ndahani alisema Rais John Magufuli anaipenda sana Singida, na ndio maana hivi karibuni amekabidhi shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa sekondari hiyo ya Utaho.
Alisema juhudi za kukabiliana na changamoto nyingine zilizopo, ikiwemo uhaba wa nyumba za walimu na maabara vitaendelea kuzingatiwa na kushughulikiwa ipasavyo, ili kuhakikisha Utaho naendelea kuwa kitovu cha elimu ndani ya mkoa.
Awali, Ndahani akiwa kwenye eneo hilo la Utaho, alipata fursa ya kutembelea na kukagua mradi wa aina yake wa shamba bora la zao la embe linalomilikiwa na mwekezaji mzawa, Aqlan Gharib maarufu “Turu Best” na aliwasihi wana-singida kwenda kujifunza teknolojia za kilimo hicho chenye tija kwa ustawi wa lishe na ongezeko la kipato.