Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozana na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai wakiwasili katika sherehe za kuwaapisha Wabunge wanne wa Chama cha ACT Wazalendo tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akimuapisha Mbunge wa Mtambwe kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Khalifa Mhamed Issa tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai
Spika wa Bunge, Job Ndugai akimuapisha Mbunge wa Wete kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Omar Ali Omar tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Bunge ambao ni wanakwaya wakiimba wimbo wa Taifa katika sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wanne wa Chama cha ACT Wazalendo tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na wageni mbali mbali pamoja na watumishi wa ofisi ya Bunge baada ya kuwaapisha Wabunge wanne wa Chama cha ACT Wazalendo tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akimuapisha Mbunge wa Chonga kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Salum Mhamed Shafi tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Mbunge wa Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Hatibu Said Haji akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na wageni mbali mbali pamoja na watumishi wa ofisi ya Bunge baada ya kuapishwa kwa Wabunge wanne wa Chama cha ACT Wazalendo tukio lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.