************************************
Klabu ya Simba imefanikiwa kuondoka na pointi tatu dhidi ya Mbeya City kwenye dimba la Sokoine mjini Mbeya baada ya kuwachapa bao 1-0.
Goli la Simba liliwekwa kimyani na Mshambuliaji John Bocco ambaye alifunga goli lake la nne la ligi kuu msimu huu.