
************************************
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 10 KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI YAKIWEMO YA KUPATIKANA NA MALI ZA WIZI NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia AMBOKILE LUCAS [20] Mkazi wa Saza akiwa na Pikipiki yenye namba za usajili MC.793 CSH aina ya Kinglion rangi nyekundu mali ya wizi.
Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 11.12.2020 majira ya saa 13:20 mchana huko Mbalizi II, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini. Mtuhumiwa amehojiwa na kuonekana hana nyaraka zozote zinazoonyesha uhalali wa kumiliki Pikipiki hiyo. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SIKUJUA OBASI [19] Mkazi wa ZZK – Mji Mdogo wa Mbalizi akiwa na pombe haramu ya Moshi @ Gongo lita 05 pamoja na mtambo mmoja wa kutengenezea pombe hiyo haramu.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 11.12.2020 majira ya saa 12:30 mchana huko maeneo ya Mlima Reli, Kata ya Utengule Usongwe, Wilaya ya Mbeya vijijini. Mtuhumiwa ni mtengenezaji, muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO.
Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa watatu 1. YUSUPH SEGERETI @ MASUBA [54] 2. GEOFREY MWANGOSI [38] na 3. ATUFWIGWEGE OSCAR [38] wote wakazi wa Kyimo Wilaya ya Rungwe wakiwa na Pombe Moshi lita 16.
Watuhumiwa walikamatwa tarehe 11.12.2020 majira ya saa 13:30 mchana huko Kijiji na Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa pombe hiyo.
KUKAMATA POMBE HARAMU YA MOSHI @ GONGO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kukamata Pombe haramu ya Moshi @ Gongo lita 40 na Pikipiki namba MC.587 CLM aina ya Boxer Bajaj BM 150 katika msako uliofanyika tarehe 11.12.2020 majira ya saa 11:30 asubuhi huko Kijiji na Kata ya Katumbasongwe, Wilaya ya Kyela.
Mtuhumiwa alikimbia mara baada ya kuwaona askari na kutelekeza Pikipiki hiyo pamoja na Pombe Moshi kiasi cha lita 40 ambayo alikuwa ameihifadhi kwenye madumu mawili ya lita 20. Msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. ALEX HEZRON [21] na 2. IBRAHIM HEZRON [19] wote wakazi wa Sae Jijini Mbeya wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi gramu 65.
Watuhumiwa walikamatwa tarehe 11.12.2020 majira ya saa 10:30 asubuhi huko maeneo ya Sae, Kata ya Ilomba, Jijini Mbeya. Watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. TUBONE ROBERT [35] Mkazi wa Ipinda na 2. MUSA AYOUB [28] Mwalimu Shule ya Msingi Mahenge na Mkazi wa Ipinda Wilaya ya Kyela wakiwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini aina ya WIN [Alcohol 41%] boksi 20.
Watuhumiwa walikamatwa tarehe 12.12.2020 majira ya saa 02:00 usiku huko Ipinda, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela katika misako inayoendelea maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.