

***********************************
Biharamulo.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya Biharamuro wamekula kiapo kwaajili ya kuanza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi wa halmashauri hiyo pamoja na kumchagua mwenyekiti na makamuĀ mwenyekiti wa baraza hilo la madiwani.
Waliochaguliwa niĀ Mhe. Rushau Leo Mathew diwani kata ya Nyanza ambaye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Biharamulo huku Mhe. Mihayo Miganyalo Lutambi diwani kata ya Nemba akichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
