Afisa Uhusiano wa TAKUKURU Doreen Kapwani,akitoa elimu kwa waandishi wa habari jijini Dodoma jinsi ya kuandika kwa ufasaha bila kupotosha habari kuhusu Utafiti wa Rushwa ya Ngono uliofanywa na taasisi hiyo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Mkurugenzi Uzuaiji Rushwa TAKUKURU Bi.Sabina Seja,akizungumza kwenye kikao cha waandishi wa habari na Viongozi wa TAKUKURU
Afisa wa TAKUKURU Bw.Juwenary John ,akitoa utafiti kwa waandishi wa habari jijini Dodoma walioufanya kuhusu Rushwa ya Ngono katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt.Ombeni Msuya,akielezea mikakati mbalimbali iliyowekwa chuoni hapo kupambana na Rushwa ya Ngono.
Mkurugenzi Taasisi ya Taaluma za Jinsia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Lulu Mahai,akizungumzia mikakati mbalimbali iliyowekwa chuoni hapo kupambana na Rushwa ya Ngono.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina ya mkutano ulioitishwa na TAKUKURU kwa waandishi hao uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mwaandishi wa Gazeti la Daily News Katare Mbashiru akiuliza Swali wakati wa Kikao cha waandishi wa habari na viongozi wa TAKUKURU jijini Dodoma
Mwaandishi wa Gazeti la Habari Leo Magnus Mahenge,akichangia maada wakati wa
Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TAKUKURU mara baada ya kuwapatia Elimu kuhusu masuala ya rushwa ya ngono vyuoni iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naye Mkurugenzi wa Tasisi ya huduma za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM Lulu Muhai amesema wamefungua ukusanjaji wa taarifa kwa kuwa na namba ya simu kwa wanafunzi kupiga simu pindi wanapokutana na changamoto ya rushwa ya ngono kwa wahadhiri wao.
Pia amesema wameaajiri wafanyakazi 36 wa jinsia zote wakike na wanaume ambao kazi yao kubwa ni kupokea malalamiko kwa wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi,na pia tumeandaa vipeperushi vinavyoelezea uadilifu.
Kwa Upande wake Afisa Takukuru Juwenary John amesema zipo sababu nyingi zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono.
Amesema Katika utafiti uliofanywa katika Taasisi za elimu ya juu vyuo vikuu viwili Chuo Kikuu cha Dar Es salaam (UDSM)na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) sababu zinazosababisha ni pamoja na Mmomonyoko wa maadili,matumizi mabaya ya madalaka,mikakati dhaifu ya kutekeleza sheria za rushwa ya ngono na uelewa hafifu.
“Hii inasababisha waathiriwa wa rushwa ya ngono kuendelea kuumia kimya kimyaa ambapo wakosaji kuendelea na vitendo hivi bila kuchukuliwa hatua stahiki za sheria,”Amesema John.
Amesema ni Tafiti zinabaini kwamba tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo vya elimu ya juu na vilivyoshiriki lipo na tatizo hili ni kubwa na si lakupuuza kwani Shuhuda za waathirika zimetambuliwa.
Aidha amesema rushwa ya ngono hugeuza haki ya muombwaji kuwa upendeleo na sio stahiki kwani inahusu kumpokonya mtu haki yake,kusababisha madhara kwenye nyanja mbalimbali kama vile kupata jelaha lisilo tibika kwenye maisha yake hata pahala pengine.
” Muhanga anaweza kugeuzwa mtumwa wa ngono,hivyo kushindwa kukuza vipaji vyake vya uhalisia ni ukweli usiopingika hali hii huathiri uchumi wa taifa,” amesema Afisa huyo Takukuru John.