Kaimu Afisa Mfawidhi Kitengo cha Udhibiti Ubora na Masoko ya mazao ya Uvuvi Bw. Frank Kabitina akifafanua namna matumizi ya barafu yanavyoongeza thamani ya mazao ya uvuvi wakati wa mafunzo ya matumizi ya barafu kwa ajili ya kuhifadhia samaki yaliyotolewa kwa wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa mazao hayo leo (03.12.2020) kwenye ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) mkoani Kigoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kituo cha Kigoma Bw. Huruma Mgana akitoa elimu juu ya faida za matumizi ya barafu kwa ajili ya kuhifadhia samaki kwa wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa zao hilo la uvuvi leo (03.12.2020) kwenye ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) mkoani Kigoma.
Baadhi ya wadau wa mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya namna barafu inavyoweza kutumika kuhifadhia samaki yaliyotolewa leo (03.12.2020) kwenye ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) mkoani Kigoma.