Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwasihi Wasanii wa Bongo Fleva kuandaa mambo ya msingi ambayo wangetaka Serikali iwasaidie ili kuendeleza tasnia ya hiyo, leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na wadau hao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katibu Mtendaji Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) Doreen Sinare akiwaeleza wasanii wa Bongo Fleva kuhusu kuongezeka kwa faini mbalimbali kwa makosa ya uharamia wa kazi za wasanii pamoja na marekebisho mbalimbali yaliyofanyika katika Kanuni ili kusaidia ongezeko la ukusanyaji wa mirabaha ya kazi za Wasanii, leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na wadau hao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii wa Bongo Fleva waliyohudhuria kikao cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya, kujadili mikakati ya kuendeleza tasnia hiyo leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam,.
Msanii wa Singeli Snura Mushi akitoa ombi kwa Serikali la kuzifuatilia Online Televisheni ili kuacha kutangaza habari zisizona na maadili kwa ajili ya kutafuta “kiki” leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika katika kikao na wadau hao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Msanii wa Hippop Niki wa Pili akitoa maoni kwa Serikali kuhusu kufuatilia majukwaa ya kidijitali ya usambazaji wa Muziki ili wasanii waweze kunufaika na kazi zao kwa kumtafuta (aggrigetor) wakitanzania atakayesimamia hilo, badala ya kuwatumia mawakala wa nje, leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika katika kikao na wadau hao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Msanii wa Taarab Mzee Yusuph akitoa ombi kwa Serikali kutafuta suluhisho la uharamia wa kazi za wasanii zinazofanywa kwa kudurufu katika CD na DVD leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na wadau hao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Msanii wa Singeli Shollo Mwamba akishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuendeleza sekta ya Sanaa na kuahidi kuvalia mavazi ya kiafrika katika ‘show’ zake zote, leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na wadau hao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Msanii wa Mashairi Mrisho Mpoto akiiomba Serikali kuanzisha matamasha ya utamaduni na mashindano ya ushairi na ili kuweza kuendeleza sanaa hiyo kwa watoto, leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kujadili mikakati ya kuendeleza sekta ya Sanaa kufuatia tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
……………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amewataka Wasanii wa Bongo Fleva kuandaa mambo muhimu wanayotaka Serikali iwafanyie ili kuboresha tasnia hiyo.
Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo Leo Desemba 1, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika kikao na Wasanii wa Bongo Fleva nchini, ambapo kikao hicho kililenga kujadilia namna bora ya kuisaidia tasnia hiyo kunufaika na kazi zake na kuweka mikakati bora ya kukuza kuendeleza tasnia hiyo.
“Katika Hotuba ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa Bunge ya alieleza azma ya Serikali kuendeleza tasnia ya Sanaa, hivyo basi ni jukumu lenu kama wadau kutoa ushauri wa nini kifanyike ili kuendeleza tasnia yenu kwani Serikali ya awamu ya tano inataka kuacha alama katika sekta ya sanaa,” alisema Dkt. Abbasi.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho cha wadau hao ambacho ni sehemu ya ziara yake ya kukutana na makundi mbalimbali ya Sanaa Dkt.Abbasi aliwasihi wasanii hao wa kutoa hoja kwani wao ndiyo wanaofahamu kwa undani changamoto zinazokwamisha mafanikio katika uendeshaji wa shughuli za muziki nchini.
“Serikali hii ya Awamu ya Tano inawathamini sana Wasanii na itaendelea kufanya kazi nanyi kwa pamoja ila ni lazima nanyi mjithamini na kuwa wazalendo,” alisema Dkt.Abbasi.
Pamoja na hayo Katika Mkuu huyo na Msemaji Mkuu wa Serikali aliwasisitiza wasanii hao kuacha kuwa na maugomvi na kuzingatia maadili.
Akizungumza kuhusu mikakati ya Serikali katika kuendeleza tasnia ya Sanaa Dkt.Abbasi alisema kuwa tayari wamempatia mtaalamu wa kuchora ramani ya kisasa ya Jengo la “Arts Arena” ambalo litakuwa la kisasa na litasaidia kufanya shughuli za Sanaa ikiwemo matamasha makubwa.
Pamoja na hayo naye Katibu Mtendaji Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA) Doreen Sinare alieleza serikali katika kupambana na masuala ya uharamia wa kazi za wasanii imeongeza malipo ya faini na kufikia zaidi ya milioni ishirini, pia kuna maboresho mbalimbali yamefanyika katika Kanuni kwa ajili ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mirabaha ya kazi za wasanii.
Halikadhalika nae Msanii wa HipPop Niki wa Pili alitoa maoni kwa Serikali kuangalia namna ya kutafuta mzawa ambaye atashughulikia usimamizi wa ukusanyaji wa wasambazaji na mauzo ya nyimbo za wasanii katika “digital platform” ili kuweza kumsaidia msanii kunufaika na kazi yake kwa wakati.
Hata hivyo nae mmoja wa Wasanii Bongo Fleva Msami Jovian alitoa ombi kwa Serikali kuangalia Online TV kwani zimekuwa zikitumika kutangaza mambo yasiyo na maadili kwa ajili ya kutoa “kiki”.
Akihitimisha mkutano huo Dkt.Abbasi aliwaeleza wasanii hao kuwa tayari Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni upo tayari na wajumbe wa bodi yake tayari wameshateuliwa, na unatarajiwa kuzinduliwa mara baada ya uteuzi wa Waziri wa wizara hiyo.
Pia alisema mapema mwanzoni mwa mwaka ujao wizara yake itaandaa tuzo kwa ajili ya wasanii kwa lengo la kutoa motisha kwa kazi wanazozifanya pamoja na kutoa fursa kwa wasanii kuwa wabunifu zaidi.
*************MWISHO************* |