…………………………………………………………………………….
NJOMBE
Ikiwa myezi miwili imepita tangu bweni la wasichana la shule ya sekondari Igima Wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe liteketee kwa moto ,Shirika la nyumba nchini NHC limetekeleza sera ya kurejesha kwa jamii kwa kuchangia zaidi ya tani 12 ambayo ni sawa na mifuko ya saruji 250 ili kufanikisha haraka ujenzi wa bweni jipya la wasichana ambao kwasasa wanalala madarasani.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo meneja wa NHC mikoa ya Njombe,Iringa na Mbeya Said Bungara anasema mapema baada ya kupokea taarifa za kuungua kwa bweni hilo wakalazimika kuanza mchakato wa kutoa mchango wao ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi za ujenzi wa bweni jipya katika shule hiyo.
Awali mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Edes Lukoa anasema ujenzi huo ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya mil 75 hadi kukamilika kwake ulisimama kipindi ambacho saruji iliadimika huku mkuu wa wilaya hiyo Lauteri Kanoni akitoa agizo kwa viongozi wa kata ya Igima na wilaya kusimamia mchakato wa michango ya wananchi ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati.
Lakini wanafunzi shuleni hapo akiwemo Mika Mbembati ambao sasa wanalazimika kulala madarasani wanazungumziaje mwenendo wa ujenzi wa bweni hilo pamoja na msaada uliotolewa ambapo wanasema utasaidia kuwamalizia shida hiyo.
Shule ya sekondari Igima iliteketea kwa moto September 15 .