Kauli hiyo ameitoa jana wakati akikakabidhi pikipiki 12 kwa masheha wa shehia za mkoa huo zenye thamani ya sh.milioni 26 ambapo alisema pikipiki hizo zitawarahisishia kazi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mbunge huyo alisema kuwa kitendo cha utoaji wa pikipiki umekuja baada ya kuona changamoto zilizojitokeza kipindi cha kampeni katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema katika kipindi hicho cha kampeni masheha hao walikuwa hawana taarifa rasmi kutokana na kuwa kila mara taarifa zinabadilika na ndipo alipoona haja ya kuwapatia vitendea kazi hizo ili kuwawezesha kuzunguka kwenye maeneo yao yote ili kuwa na taarifa rasmi.
Mbunge huyo alisema pikipiki hizo zimetolewa kwa wilaya ambapo pikipiki tano zilitolewa kwa masheha wa wilaya ya Kaskazini ‘A’ na wilaya ya Kaskazini ‘B’ katika mkoa huo wa Kaskazini Unguja kutokana na kuwa maeneo yao ni makubwa na hawana vitendea kazi.
“Tunapohitaji taarifa zinazohusu shehia zao huwa zinachelewa au zimekuja bila ya uhalisia hivyo mategemeo yetu pikipiki hichi zitatufanya tupate taarifa kwa wakati,” alisema
Alisema pikipiki hizo zitawapa nafasi za kufanya kazi na kupeleka kupata taarifa kwa wakati sambamba na kujenga mahusiano haina ya viongozi wa Chama na serikali.
“Masheha ni viongozi wa Serikali hivyo kutaweza kuwasaidia wananchi kwa ukaribu zaidi kwani masheha ni viongozi wa Serikali nasi tunawasaidia katika kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema
Hata hivyo, aliwataka masheha hao kuzitumia kwa uangalifu kwa kuvaa kofia ngumu ‘helmenti’ na kuendesha kwa mwendo wa kawaida ili kuweza kuepusha ajali zilizokuwa si za lazima pamoja na kufuata sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Kaskazini Unguja, Maryam Muharami Shomari, alisema kutolewa kwa pikipiki hizo, zinaonyesha wazi kuwa Mbunge huyo anatambua umuhimu wa masheha kutokana na kumekuwepo kwa umuhimu wa sheha katika kufanya kazi zao kwa umakini.
Pia, aliwataka Wabunge wengine kuendeleza aliyoyaanza Mbunge huyo ili kuweza kukamilisha idadi ya masheha waliokuwepo katika Mkoa huo kupata vitendea kazi katika Mkoa na wilaya zao.
Naye sheha wa shehia ya Matemwe, Vuai Faraji Mcha, alisema amefarijika kupatiwa pikipiki hizo na kwamba kuahidi kuitumia pikipiki hizo kuwa lengo lilokusudiwa ili kuona hali ya kiutendaji inakwenda kama ilivyopangwa pamoja na kumuahidi mbunge huyo kufanya kazi kwa lengo la kupatiwa.