Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 Samwel Humbe aliyeshinda Sh145,351,400 na kuwa mshindi wa 94 tokea kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2017. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha michezo ya kubahatisha mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga.
**************************************
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la ‘Ni Zamu Yako’ ambayo imekwenda sambamba na kukabidhi zawadi ya mshindi wa 94 wa Perfect 12, Samwel Humbe ambaye alizawadiwa Sh145,351,400.
Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa kampeni hiyo inahamasisha mashabiki wa soka na watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 kuendelea kubashiri na kuwa miongoni mwa washindi ambao watajishindia mamilioni ya fedha kupitia mchezo wa Perfect 12 na michezo mingine ya kubahatisha ya kampuni hiyo.
Mushi alisema kuwa mpaka sasa wametumia Sh4.2 billioni kuwazadia washindi mbalimbali kupitia mchezo wa Perfect 12 ambayo ulianza rasmi mwaka 2017.
“Humbe ni mshindi wa 94 tokea kuanza kwa mchezo huo wa kubahatisha wa Perfect 12 ambao umeweza kubadili maisha ya Watanzania wengi hapa nchini. Kampeni mpya inahamasisha zaidi mashabiki kuendelea ‘kubeti’ kupitia M-Bet ambayo kwa sasa imeweza kuwapa maendeleo mashabiki wa soka na kujiunga na nyumba ya mabingwa,” alisema Mushi.
Kwa upande wake, Humbe ambaye ni shabiki wa Yanga alisema kuwa atatumia fedha hizo kunzisha biashara mpya huku akiwasomesha watoto wake.
Alisema kuwa pia ataendeleza kazi yake ya ufundi selemala kwa kununua vifaa vya kisasa na kuifanya kazi yake iwe ya kisasa.
“Nimefurahi sana kushinda, sikuamini kupata ushindi huu ambao kwa ujumla, naipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa wakweli na mshindi anapatikana kwa mujibu wa sheria,” alisema Humbe.
Mkuu wa kitengo cha michezo ya kubahatisha mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga alimpongeza Humbe kwa ushindi na kampuni ya M-Bet kwa kutimiza wajibu wake ikiwa pamoja na kulipa kodi za serikali.