Programu hiyo iliyopewa jina la Dar Largest Swimming lesson ilizinduliwa Jumamosi ambapo wanafunzi mbalimbali kutoka shule tofauti za Msingi mkoani Dar es Salaam walishiriki na kuanza mafunzo hayo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Romeo alisema kuwa ameamua kuanzisha program hiyo kama semehu ya kutafuta vipaji miongoni mwa watoto ambao kwa namna moja au nyingine, wanashindwa kupata mafunzo hayo kutokana na changamoto mbalimbali.
Alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa bure na mipango yao ni kuyafanya mara moja kwa kila mwaka huku mipango mbioni kuendesha mafunzo hayo kwa kila mwezi.
“Mimi nimejifunza kuogelea kutokana na sapoti kutoka kwa wazazi wangu, naomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kujifunza kuogelea ili kujua vipaji vyao na vile vile kupata nafasi ya kujilinda na majanga ya maji.
Hivi karibuni, familia nyingi ziliathirika na mafuriko na baadhi ya watu kupoteza maisha kutokana na kuzolewa na maji. Lakini kama wangekuwa wanajua kuogelea, wasingeweza poteza maisha yao. Nimeona changamoto hiyo na ndiyo maana nimeamua kuanzisha mafunzo haya,” alisema Romea.
Alisema kuwa mbali yay eye kuwa miongoni mwa watoa mafunzo, pia makocha wa timu ya Champion Rise watakuwa wanashiriki katika mafunzo hayo ambayo katika uzinduzi, yalidhaminiwa na kampuni ya Pepsi.