NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga imeendelea kutembezea kichapo katika ligi Kuu Tanzania bara baada ya leo hii kuichapa JKT Tanzania bao 1-0 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Yanga lilifungwa na yule yule ambaye alipeleka kilio Chamanzi hivi karibu ni Deusi Kaseke akiingia kambani dakika ya 33 ya mchezo na goli hilo kudumu mpaka mwisho wa mchezo.
Yanga imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa imeshuka dimba mara 13 na kujinyakulia pointi 31 na kongoza ligi huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Azam Fc ambayo imeshuka dimbani mara 12 na kufanikiwa kuwa na pointi 25.