*******************************************
Wakulima wa mkoa wa Katavi wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za kifedha katika kuchukua mikopo ya pembejeo ili kuinua kuwawezesha kufanya kilimo biashara na kukuza pato lao
Rai hiyo imetolewa na meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mpanda – Alex Massawe wakati akifungua mkutano maalum na wakulima na wafanyabishara wa mkoa huo.
Massawe amesema Benki ya NMB imekuwa ikikutana na wakulima wa maeneo tofauti kwa lengo la kutoa elimu ya kilimo biashara ambayo itamsaidia mkulima kuleta tija katika kilimo.
Akizungumzia mikopo hiyo ya pembejeo, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo Biashara Wogofya Mfalamagoha amesema NMB inatoa mikopo ya pembejeo za aina tofauti kwa wakulima ambapo rejesho lake ni mara moja tu kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu.
Aidha Mwakilishi kutoka NMB foundation – Rogers Shipela amethibitisha kuwa taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima
“Taasisi ya NMB foundation imeundwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambapo mkulima ataweza kuuza mazao yake kwa bei itakayomnufaisha pamoja na hilo tunatoa elimu ya masoko ambayo inatolewa ili mkulima aweze kuuza mazao yake kwa ufanisi “alisema