Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizindua GBV APP kwa ajili ya kupata taarifa za Ukatili wa Kijinsia wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam kulia mwenye koti ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya – Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya – Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea utekelezaji wa Afua mbalimbali za Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akiangalia muonekano wa GBV APP iliyotengenezwa kwa ajili ya kupata taarifa za Ukatili wa Kijinsia wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto jijini Dar es Salaam kulia mwenye koti ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya – Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja pamoja na wanaharakati wa Mapambano dhidi ya Ukatili wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam wa pili kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia masuala mbalimbali katika Uzinduzi wa Siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto jijini Dar es Salaam.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
***********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Serikali inaendelea na mikakati ya kuhakikisha inapambana na Kutokomeza vitendo vya Ukatili wa kijinsia kupitia mpango wa kamati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini ambao umelenga ifikapo 2022 Vitendo hivyo viwe vimepungua kwa asilimia 50.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson wakati akizindua Kampeni ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia ikiongozwa na Kauli mbiu isemayo “Tupinge vitendo vya Ukatili Mabadiliko yananza na mimi” uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia utekekezaji wa Mipango mbalimbali ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau katika kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na Watoto vinatokomezwa nchini.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake, Sheria na Maendeleo-Wildaf Bi.Anna Kulaya amesema kuwa Wanawake wa vijijini na hasa wenye elimu duni wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili hivyo jitihada kubwa zinahitajika katika kuhakikisha Jamii hiyo inapata elimu ya kutokomeza vitendo vya kikatili.
Katika hatua nyinge Dkt.Tulia Ackson amezindua GBV APP maalumu kwa ajili ya wananchi kupata taarifa mbalimbali kuhusu vitendo vya ukatili ikiwemo elimu juu ya mapambano dhidi ya vitendo hivyo.