…………………………………………………
Na John Walter, Babati
Wafanyakazi Wa Kampuni Ya Usimikaji Wa Nguzo Kubwa za Umeme (Tower) Bouygues Energies Service Wamegoma Kuendelea Na Kazi Kufuatia Madai Yao Wanayodai Kwa zaidi Ya Mwaka Mmoja.
Kampuni hiyo ni Miongoni mwa Kampuni tatu ambazo Oktoba 7, 2016 Makao Makuu ya TANESCO Jijini Dar es Salaam, zilisaini mikataba na Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), ya Msongo wa Kilovolti 400 Tanzania na utakaounganisha Kenya.
Kampuni zingine ambazo ziliingia makubaliano na kutia saini ni Energoinvest na Kalpa-Taru.
Wafanyakazi hao wamesema kuwa wengine wamehamishwa Kutoka Mikoa Mbalimbali ili kuja kufanya kazi katika Kampuni kwenye eneo la mradi uliopo eneo la Magugu wilaya ya Babati Mkoani Manyara kwa makubaliano kuwamba wangeongezwa kiasi cha mshahara lakini matokeo yake kampuni imefanya kinyume na makubaliano.
Kwa mantiki hiyo Wafanyakazi wote wameamua kugoma Kufanya kazi wakisubiri majibu kutoka kwa Uongozi wa Kampuni hiyo kuhusu madai yao yanayolenga kulipwa mafao yao waliyokuwa wanakatwa.
Hata hivyo Uongozi Wa Kampuni hiyo ulipotafutwa Kuzungumzia suala hilo uligoma kutoa Ushirikiano Kwa Waandishi wa Habari na hata alipotafutwa Kwa njia ya Simu Amiri Shio Afisa Rasilimali Watu Wa Kampuni hiyo alisema Kuwa hana taarifa kuhusu Madai hayo na kwamba hawezi Kuzungumza Chochote.
Wafanyakazi hao wameeleza kuwa wanasubiri majibu Kutoka Kwenye Kampuni hiyo huku Wakitafuta Mwanasheria atakaewasaidia Kutatua Suala Hilo Kisheria.
Kiongozi Wa Wafanyakazi Hao Bwana Laizer aliwatuliza Wafanyakazi hao na Kuwataka wasubiri pindi wanapofuatilia Suala Hilo.
Wameeleza Kuwa Kwa Siku Wanalipwa Shilingi Mia Saba ya Chakula na baada ya Kulalamika wameongezewa Shilingi Mia tatu huku wakiingia kazini saa moja asubuhi na kutoka saa kumi na moja jioni na wakati mwingine hadi saa kumi na mbili jioni.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Mhandishi Alexander Kyaruzi akizungumzia mradi huo Machi 27,2019 alisema mradi mzima una urefu wa kilomita 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni Isinya Kenya hadi Namanga Kilomita kilomita 96, sehemu ya pili unahusu Namanga- Arusha Kilomita 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilomita 150, na Babati-Singida kilomita 150.