**********************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa kampuni ya CICO anayetekeleza Mradi wa ujezi wa Daraja la Ulongoni “A” ambalo Ujenzi wake umekuwa ukisuasua jambo linalosababisha usumbufu kwa wakazi wa Ulongoni.
Kutokana na hilo RC Kunenge ametoa agizo kwa mkandarasi, mshauri Mradi,mratibu wa DMDP kufika ofisini kwake Jumatano ya November 25 huku akimuelekeza meneja wa TANROAD Mkoa kumpatia Mtaalamu wa kufanya ufuatiliaji na uchunguzi wa utendaji kazi tangu kuanza kwa Mradi huo Hadi sasa.
Aidha RC Kunenge amesema kitendo Cha uzembe wa mkandarasi huyo ni uchonganishi baina ya wananchi na Serikali yao ambayo iliahidi kujenga Daraja hilo na tayari Serikali ilishatoa fedha za Ujenzi huo lakini mkandarasi amekuwa akikwamisha juhudi hizo.
Hata hivyo RC Kunenge amepinga sababu zilizotolewa na mkandarasi huyo kuwa Ujenzi umechelewa sababu ya Corona na Mvua wakati miradi kwenye maeneo mengine inaendelea Kama kawaida akitolea mfano wa Ujenzi wa Daraja la Tanzanite linalopita katikati ya bahari.
Nao baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kukosekana kwa Daraja imekuwa kilio kikubwa kwao na kueleza kuwa baadhi ya watu wamefariki dunia kwa kuchukuliwa na maji kipindi Cha mvua wakirajibu kuvuka.