Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Fainali za shindano la urembo la Miss Tanzania litakalofanyika tarehe 5 Desemba 2020 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Yenye kauli mbiu ya ‘urembo ni heshima’
Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look Bi. Basilla Mwanukuzi ambao ndio waandaaji na waratibu wa shindano hilo kubwa lenye hadhi hapa nchini amejulisha Vyombo vya Habari kwamba Mheshimiwa Tulia Ackson amethibitisha kuwa Mgeni Rasmi wa shindano hilo.
Hii ni mara ya tatu mfululizo Kampuni ya The Look inaandaa shindano hilo tangu mwaka 2018 walipochukua umiliki kutoka kwa waandaali wa mwanzo. Naibu Spika Mheshimiwa Tulia Ackson ni mwanamichezo, mpenda sanaa na kinara katika shughuli zinazoweka kipaumbele katika kusaidia jamii na amekuwa akifuatilia kwa karibu mashindano haya ambayo yanaendeshwa kwa malengo ya mashindano ya dunia ya ‘beauty with a purpose’ na yamekuwa yakitoa fursa mbalimbali kwa wasichana na wadau wengine wa tasnia ya urembo. Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, ambapo wasichana 20 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania wamefuzukuingia fainali.
Licha ya changamoto ya ugonjwa wa korona mwanzoni mwa mwaka kumekua na wito mkubwa sana wa warembo wenye vigezo vya kushiriki mashindano kujitokeza samabamba na vigezo mwaka huu warembo wote 20 wana miradi yao ya kusaidia jamii BWAP ‘Beauty with a purpose project’ ambazo nazo zitashindanishwa na project moja itaibuka kidedea.
Shindano la mwaka huu linatarajiwa kua na msisimko wa aina yake kutokana na maandalizi mazuri na warembo waliofuzu fainali kua na vigezo vya hali ya juu vya mashindano ya dunia. Warembo waliofuzu kuingia fainali ni kama ifuatavyo;-
- PRISCA LYIMO – UBUNGO DSM
- TAMIA HAKAM – ARUSHA
- JULIANA RUGUMISA – ARUSHA
- REHEMA CUTHBERT – ARUSHA
- YVONNE PAUL – KIGAMBONI
- RUTH BENITHO – ILALA
- GRACE MACHIBULA – UBUNGO
- ROSE MANFERE – TEMEKE DSM
- MARGARET MWAMBI – KIGAMBONI DSM
- SARAFINA MAGEYE – KINONDONI
- MARTHA GOLODI – UBUNGO DSM
- ZENITHA CHUNDU – MOROGORO
- DEOLYN MOLLEL – MOROGORO
- HOYCE BAKANOBA – TABORA
- NECERIAN KIVUYO – DODOMA
- RAZIA ABRAHAM – KINONDONI DSM
- ANGELA PENDAELI – ARUSHA
- ADVERA MWEMBA – MWANZA
- VERYNICE DEOKARI – KINONDONI DSM
- GLORIA FELA – ILALA DSM