NA RAHEL NYABALI
……………………………………………………………………..
KIGOMA.
Wajasiliamali na wafanya biashara wadogo wadogo Wanawake Mkoani Kgoma wameziomba taasisi za kifedha ambazo zinatoa mikopo kupunguza masharti ya utoaji na ulipaji wa mikopo hiyo ili hatua ambayo itaweza kuwasaidia kukuza mitaji yao.
Yameelezwa hayo katika semina iliyo andaliwa na Benki ya CRDB iliyo lenga kuwainua wanawake wajasiriamali, kiuchumi kuondokana na mikopo umiza waliyo kuwa wanachukua mitaani.
Eppifania kagoye na Sesilia Funga nibaadhi ya wajasilia mali mkoani humo wamesema kuwa taasisi nyingi za kifedha ambazo zinapitikana mitaani zimekuwa zikitoa riba kubwa hivyo kusababisha biashara za wanawake wengi kuzidi kudumaa .
Akisisitiza wanawake kufungua akaunti ya Malkia ambayo inatoa fursa kwa wanawake kujipatia mikopo, Rachel senni ambaye ni meneja wa huduma kwa wanawake amesema huduma hiyio itasaidia kuinua kundi kubwa la wanawake ambao walishindwa kufikia Marengo yao.
Saidi pamui ni meneja CRDB kanda ya Magharibi amesema lengo la benki hiyo ni kuunga juhudi za serikali kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ikiwa na lengo la kukuza mitaji ya wajasiriamali na wafanya biashara.