***********************************
Klabu ya Simba yainyuka Coastal Union ya Tanga mabao 7-0 kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid mjini Arusha huku tukishuhudia mkali wa mabao John Bocco akifunga Hat-Trick kwenye mchezo huo ambapo alifunga dakika 25,28 na 38.
Simba katika kipindi cha kwanza ilifanikiwa kuvuna mabao mengi kwani mpaka kufikia dakika 45 walikuwa wanaongoza mabao 5-0.
Kipindi cha pili Simba iliendelea kutafuta mabao zaidi licha kosa kosa nyingi zilitokea lakini mwisho waliibuka washindi kwa mbao 7-0.
Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Chama dakika 60,86 na bao lingine likifungwa na Hassan Dilunga mnamo dakika ya 7 ya mchezo.