************************************
21/11/2020 MTWARA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi Hilo na kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia kupambana na kikundi cha watu wanaotekeleza uhalifu katika vijiji Vya mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
IGP Sirro amesema hayo Leo wakati alipofanya ukaguzi na kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara katika vijiji Vya Kitaya na Michenjele mkoani Mtwara, vijiji ambavyo hivikaribuni vilivamiwa na wahalifu wanaodaiwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji waliochoma moto baadhi ya nyumba za watu, kuchoma moto magari na thamani nyingine pamoja na kusababisha mauaji.
Naye mkazi wa kijiji cha Michenjele Muhibu Mshamu, amevipongeza vyombo Vya Usalama kwa kuimarisha usalama katika vijiji hi you hali ambayo imesaidia kuwaondolea hofu wananchi kufuatia tukio la uvamizi.