SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai,akizungumza kwenye semina ya wabunge iliyoandaliwa na UNICEF katika maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Shirika la UN, Zlatan Milisic,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Mwakilishi wa UNICEF Bi. Shalini Bahuguna,akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Mtoto kutoka Mbeya Agape Joster (13),akiwaeleza wabunge kuwa wanakabiliwa na kero mbalimbali wakiwa mashuleni wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Abdulltif Hassan (16) kutoka shule ya Chuini Sekondari Zanzibar akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Sehemu ya wabunge wakifatilia maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Baadhi ya watoto pamoja na vijana wakifatilia majadiliano wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson,akitoa neno la shukrani kwa UNICEF baada ya kuwapa semina wabunge wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai,akiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa hotuba wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wametaka kusoma na kuzielewa ajenda za watoto pamoja na vijana ili kuisaidia serikali kutekeleza malengo endelevu SDGS.
Kauli hiyo imetolewa na Spika Job Ndugai wakati wa Semina ya wabunge iliyoandaliwa na UNICEF kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.
Ndugai amesema kuwa wabunge wanatakiwa kusoma kitabu cha ajenda za watoto na vijana kilichotolewa na shirika la kusaidia watoto Duniani UNICEF , ili kuzielewa na kuisaidia serikali kutekeleza masuala mbalimbali ambayo imesaini katika mikataba ya kimataifa.
“Bunge letu tukufu tayari lilishaingia makubaliano yaani MOU, na shirika linalojihusisha na masuala ya watoto Duniani (Unicef) katika kusaidia kupambania haki za watoto,”amesema Ndugai
Aidha, amesema kuwa Bunge lake lipo tayari kufanya kazi na mashirika mbalimbali nchini na yale ya kimataifa ili kusaidia kulinda haki za watoto na vijana.
Hata hivyo Ndugai,ametoa wito kwa shirika la Unicef kutoa elimu kwa wabunge kwa njia ya semina, mafunzo pamoja ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ili kujifunza mambo yanayohusu haki ya mtoto.
Awali Mwakilishi wa Unicef, Shalini Bahuguna amesema kuwa bado kuna kero mbalimbali zinazo wakabili watoto katika jamii ambazo serikali inatakiwa kuwekeza jitihada zaidi ili kuzitatua.
Bahuguna, amesema kuwa serikali ya Tanzania inatakiwa kuendelea kuwekeza kwa watoto ili kusaidia kuwaondolea kero mbalimbali ambazo zinachangia kukwamisha ndoto zao.
Naye Mratibu Mkazi wa Shirika la UN, Zlatan Milisic amesema kuwa anaipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazozifanya ili kulinda haki za mtoto.
Hata hivyo amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani mwaka huu yanafanyika ikiwa imepita miaka 31,toka mkataba wa kimataifa kuhusu kilinda haki za mtoto usainiwe.