Na Kadama Malunde – Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amefunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) lililokuwa linafanyika katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Novemba 18,2020 hadi leo Novemba 20,2020.
Tamasha hilo lenye Kauli Mbiu ya “Miaka 25 ya Beijing : Tusherehekee, Tutafakari, Tujipange, Tusonge Mbele, Twende pamoja” limekutanisha wadau wa haki za wanawake na watoto zaidi ya 400 kutoka mikoa 9 nchini ambayo ni Shinyanga, Mara, Tanga, Dar es salaam, Mbeya,Kilimanjaro,Dodoma, Mtwara na Kigoma.
Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo leo, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewataka wanawake kujiona ni wa thamani na kusimama imara na kuachana na mtazamo kuwa mwanaume ndiyo anatakiwa afanye kila kitu katika familia.
Chalamila amesema serikali inaendelea kuboresha hali ya maisha ya wanawake ili kufikia usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapatia mikopo kupitia halmashauri za wilaya.
“Wanawake simameni imara bila kufifisha thamani yenu, mwanamke siyo mtu wa ndiyo ndiyo tu kwa kila kitu. Msijirahishe rahishe na kukubali rushwa ya ngono.Tafuteni fursa za uongozi huku mkitambua kuwa mwanamke akiwa katika nafasi salama basi kizazi chote kimepona”,amesema Chalamila.
Mkuu huyo wa mkoa pia amekemea vitendo vya wanaume kudhulumu mali wanawake na kwamba serikali haipo tayari kuona wanawake na watoto wakionewa na kunyanyaswa huku akiwasisitiza wanawake kutoa taarifa pale wanapotendewa vitendo vya kikatili ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Katika hatua nyingine Chalamila amesema mkoa wa Mbeya bado unakumbwa na matukio ya unyanyasaji dhidi ya watoto ikiwemo ubakaji na kukata sehemu za siri za watoto matukio ambayo yanahusishwa na imani za kishirikiana hivyo kuitaka jamii kuachana na vitendo hivyo
Chalamila ametumia fursa ya Tamasha hilo kuupongeza Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa namna unavyoshirikiana na serikali katika kupigania haki za wanawake na watoto.
“TGNP mmekuwa wadau wakubwa katika mkoa wa Mbeya,mmeisaidia sana serikali kufanya mambo ambayo yalipaswa kufanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi”,amesema.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020. Wa kwanza kulia ni Chifu wa Kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya, Roketi Mwanshinga akifuatiwa na Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa akifunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila akizungumza wakati wa akifunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Mjumbe wa Bodi ya TGNP, Jovita Mlay akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya , Nicodemus Tendwa akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Wanawake na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Wanawake na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Chifu wa Kabila la Wasafwa mkoa wa Mbeya, Roketi Mwanshinga akizungumza wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Washiriki wa Tamasha la 6 la Jinsia Ngazi ya Wilaya wakicheza muziki na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila wakati wa kufunga Tamasha la sita la Jinsia Ngazi ya Wilaya lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika uwanja wa Kijiji cha Hatwelo kata ya Ijombe Halmashauri ya wilaya ya Mbeya leo Ijumaa Novemba 20,2020.
Katibu Msaidizi wa Jukwaa la Vijana Wafeminia kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Asha Nyoni akimpatia zawadi ya Tisheti Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog