Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kushoto) akihitimisha mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la 12 leo Bungeni Dodoma. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG) Ndg. Charles Kichere akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma. Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Harold Nsekela akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma.
Katibu Mstaafu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma.
PICHA NA BUNGE