………………………………………………………………………….
Kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC , kesho kitashuka Dimbani kumenyana na Azam FC katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo hadi sasa kikosi hicho kimeshafanya maandalizi ya kutosha kwa asilimia kubwa.
KMC FC ambao ni wenyeji wa mchezo huo, wamejipanga kuhakikisha kwamba licha ya wapinzani wao kuongoza ligi kuu lakini maandalizi yaliyofanyika chini ya Kaimu Kocha Mkuu, John Simkoko pamoja na kocha msaidi Habibu Kondo ya taleta matokeo mazuri katika mpambano huo.
Katika kipindi chote cha mapumziko ,KMC FC ilitumia nafasi ya kucheza mechi nyingi za kirafiki na hivyo kutoa nafasi kwa walimu kurekebisha makosa mbalimbali ambayo yalionekana katika michezo hiyo na kwamba mashabiki wategemee kupata alama tatu katika mchezo huo.
Aidha kikosi hicho kimejipanga katika muendelezo wa liki kuu mara baada ya mapumziko ya mechi za Kimataifa kumalizika kuhakikisha kwamba kinafanya vizuri kwa kila mchezo bila kupoteza.
“Katika mchezo wa kesho hakuna cha pira Icream, Stobel, wala pira mkate KMC itakwenda kuonesha pira spana ,mashabiki wajitokeze kwa wingi kuisapoti Timu yao, kikosi chetu ni kizuri hivyo azamu waje wakiwa wamejipanga wasijekutoa sababu pindi watakapofungwa.
Aidha katika mchezo wa kesho, KMC FC inakabiliwa na wachezaji wenye majeruhi wa tatu ambao ni Keneth Masumbuko, Abdul Hilary pamoja na Andrew Vicent (Dante).