*****************************
Na John Walter-Babati
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Isaka Kuppa amemhukumu kwenda jela miaka mitatu na kulipa faini ya shilingi million moja na laki tano aliyekuwa hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo ya Magugu Adeltus Richard Rweyendera.
Hukumu hiyo imetolewa tarehe 13/11/2020 baada ya waendesha mashtaka wa takukuru Martin Makami na Evelyne Onditi kuwasilisha ushahidi dhidi ya mshitakiwa Rweyendera kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 1985 ambapo mahakama ilimkuta na hatia na kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Holle Makungu alisema Rweyendera amepewa adhabu hiyo katika kesi ya rushwa namba CC .137/2020 baada ya kupatikana na hatia kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki moja na nusu (150,000) kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya 11/2007.
Holle alieleza kuwa Rweyendera aliomba fedha hizo toka kwa wazazi wa ndugu wa washitakiwa watatu ambao walikuwa wakishtakiwa kwenye kesi namba 242/2020ikiwa ni kishawishi cha kuwasaidia na kuwaachia huru wastakiwa hao kwenye kesi ambayo hakimu huyoalikuwa anaisikiliza katika mahakama ya mwanzo Magugu.
‘’Baada ya kupokea taarifa kutoka kw siri wetu ofisi yetu ilifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa ni kweli kesi hiyo ilikuwepo katika mahakama ya mwanzo ya magugu na kwamba ilikuwa inasikilizwa na hakimu Adeltus Richard Rweyendera ambapo uchunguzi wetu pia ulibaini watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma za uzururaji miongoni mwao wakiwa kwenye sehemu zao za biashara,kwa kuwa washitakiwa walikuwa watatu hakimu aliwataka wachangie elfu50 kila mmoja ambapo jumla ingekuwa laki moja na nusu”alisema Makungu.
Katika hatua nyingine takukuru Mkoani Manyara imewezesha askari wa wanyamapori Jumuiya tya hifadhi ya wanyamapori Burunge(JUHIBU)kulipwa stahiki zao zilizokuwa zimezuiliwa na spika wa jumuiya hiyo Ndg.Marcel Alfred Yeno.
Jumuiya ya Wanyamapori Burunge (WMA/JUHIBU) inajumuisha uhifadhi wa uhifadhi wa wanyamapori kwa lengo la kuinua hali ya kiuchumi na kustawisha maisha ya wanachama wake ambapo jumiya hiyo inaundwa na vijiji 10vinavyozunguka hifadhi ya wanyama pori Tarangire.
Mkuu wa takukuru mkoani hapa alieleza uchunguzi uliofanywa na takukuru ulibaini juhibu iliingia mkataba wa kazi na kampuni ya Bouygues katika mradi wa umeme wa 400kv ambao unapita karibu na eneo la hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya tarangire kuelekea Namanga ambapo katika mkataba huo walikubaliana kila askari anayekwenda lindo alipwe shilingi elfu 25 kwa siku.
Alisema kati ya tarehe 27/7/2020 na 28/8/2020 askari 17 wa juhibu walishiriki katika ulinzi wa mradi huo wakitumia mishahara yao huku wakiwa na matumaini kwamba wangelipwa mwisho wa mwezi stahiki zao kwa mujibu wa mkaba lakini hawakulipwa.
Uchunguzi umebaini kuwa kampuni ya Bouygues walilipa kiasi cha million 2 na laki 3 kwenye akaunti ya juhibu kwa ajili ya skari hao lakini spika huyo akadhuiya kuidhinisha malipo hayo na kuwalazimisha askari hao kutia sahihi karatasi za malipo ili kuonyesha kuwa wamelipwa na kudai kwamba wale ambao wangekataa angewapeleka kwenye kazi cha kuwaazimia kufukuzwa kazi.
Makungu alisema kitendo hicho kilichofanywa na spika Marcel ni matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha sheria cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya 2007 hivyo baada ya takukuru kuingilia kati kwa askari kulipwa haki zao pia wamemtaka spika huyo ajipime iwapo anastahili kuendelea kuiongoza juhibu kabla hajachukuliwa hatua.