***************************************
Na John Walter-Manyara
Siku ya tarehe 19 Novemba ya kila mwaka ni ‘Siku ya Matumizi ya Choo Duniani’. (World Toilet Day).
Lengo la siku hii ni kuwaleta wadau mbalimbali kufahamu umuhimu wa kuwa na choo bora na vyombo vya kunawa mkono na kutumia.
Afisa afya mkoa wa Manyara Evance Semkoko akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa katika kaya walizozitembelea mkoani hapo, wamebaini kuwa asilimia 12 ya kaya hazina vyoo.
Katika siku ya choo duniani, afisa afya mkoa wa Manyara Evance Semkoko, amesema takwimu zinaonyesha bado asilimia 12 ya watu mkoa wa Manyara hawana huduma hii ya msingi, huku shirika la afya duniani WHO, likitoa wito wa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa wote endapo tunataka kutimiza malengo ya afya ifikapo 2030.
Semkoko amesema pamoja na mambo mengine siku ya choo duniani inawakumbusha wananchi kuwa na vyoo bora ili kuepuka maradhi yanayotokana na kusambaa kwa kinyesi na Kuwa na uchumi endelevu.
Ameeleza kuwa Choo ni muhimu kwa sababu binadamu anapojisaidia kinyesi chake kinakuwa na vimelea vingi vya magonjwa ambavyo huleta mlipuko wa magonjwa mbalimbali.
Ameongeza kuwa “ni vigumu binadamu kukila kinyesi lakini anakitumia kinyesi hicho bila kujua kutokana na vitu vinavyosambaza vimelea hivyo akitolea mfano Nzi, kutokunawa mikono baada ya kutoka chooni”
Vyoo vinaokoa maisha kwa sababu kusambaa kwa kinyesi cha binadamu kunasababisha maradhi mengi yanayoweza kukatisha maisha ya watu kila mwaka ulisema Umoja wa Mataifa mwaka 2019 katika siku ya choo duniani.
Kauli mbiu ya Siku ya Choo Duniani kwa mwaka 2020 inasema “Tuzingatie jinsia katika kuhamasisha usafi wa mazingira ili tuwe na usafi endelevu”.
Tanzania inaungana na Nchi mbalimbali kuazimisha siku hii ambapo elimu kwa njia mbalimbali hutolewa, ukaguzi katika ngazi ya kaya na kufanya makongamano mbalimbali.
Attachments area