Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waandishi wa habari nchini na wananchi wameombwa kutumia mfumo wa kidigitali wa kutoa taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu uitwao “Haki Kiganjani” wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486.
Wito huo umetolewa na Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James wakati mafunzo ya Sheria za Uhuru wa Habari kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa (Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera na Mara) ili kuwajengea uwezo kuzielewa sheria zinazoongoza Tasnia ya Habari nchini.
Nikumwitika amewashauri waandishi wa habari kutumia mfuko mfumo wa kidigitali kutoa taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu wanayokutana nayo lakini pia watoe elimu kwa wananchi Jinsi ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ kwa kutumia simu janja au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi SMS) kwenda namba 0699695486.
“Watu wana matatizo lakini hawajui wayapeleke wapi, wayaripoti wapi. Naomba mtusaidie kuwapa namba hii ya simu 0699695486 ya simu watume sms/ujumbe au muwafahamishe kupakua/Ku – download App ya ‘Haki Kiganjani’ iliyopo Playstore ambayo itawezesha kutuma taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu”,amesema.
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale amesema mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha waandishi wa habari kuzijua sheria zinazohusu tasnia ya habari ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.
“Lengo la LHRC imetoa mafunzo haya katika Kanda saba nchini na kwa muda wa siku mbili tumetoa kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa ili kuboresha uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari”,amesema.
“Kutokana na utungwaji na mabadiliko mbalimbali ya sheria za wanahabari LHRC imewajengea uwezo waandishi wa habari juu ya sheria mbalimbali zinazoongoza tasnia ya habari ili kupunguza changamoto zitokanazo na ukiukwaji wa sheria kwa waandishi wa habari”,ameongeza Ntwale.
Amesema mbali na kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika sheria za uhuru wa kujieleza pia wametoa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa kidigitali wa kutoa taarifa za matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ujulikanao kama ‘Haki Kiganjani’.
Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.
Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ au simu ya kawaida kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0699 695 486 kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.
Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James akitoa mada kuhusu namna ya kutumia Application ya ‘Haki Kiganjani’ wakitumia simu janja ‘smartphone’ kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu leo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa.

Wakili wa Kujitegemea Pasience Mlowe akitoa ufafanuzi kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Wakili wa Kujitegemea Pasience Mlowe akitoa ufafanuzi kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari.
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akiwasihi waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia sheria.
Afisa Programu wa LHRC Wakili Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo. Kushoto ni Afisa TEHAMA wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre – LHRC), Nikumwitika James.
Mwandishi wa habari Rose Mweko kutoka mkoa wa Geita akitoa neno la shukrani kwa LHRC kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka mkoa wa Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara na Kagera kutoa mafunzo ya sheria zinazohusu tasnia ya habari.
Washiriki wa mafunzo hayo wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo ya siku mbili.
Washiriki wa mafunzo hayo wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo ya siku mbili.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog