Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa , Waziri wa Fedha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS Dkt.John Magufuli amesema kuwa hana haraka ya kuteua baraza jipya la
mawaziri kutokana na kupatikana ka wabunge wengi wa CCM wenye sifa nzuri.
Pia Rais .Magufuli amewataka wabunge hao kutokuwa na presha ya
nafasi za uwaziri kwani walichoomba ni ubunge na siyo uwaziri.
Rais Dkt.Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati wa hafla ya kumupiasha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip
Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof.a Palamagamba Kabudi Ikulu Chamwino Dodoma.
Rais Magufuli amesema kuwa kuna wabunge zaidi ya 350 mpaka sasa na
bado wabunge wengine sijawateuliwa hivyo inahitaji nafasi na kuchambua
kwa kina katika kuwapata mawaziri.
” Sikua na haraka ya kuteua safari hii tuna wabunge zaidi ya 350 bado wale 10 wa nafasi zangu, hawa wawili ni kwa sababu wabunge inabidi mlipwe mshahara na miradi mingine iendelee ndio maana nimechagua Waziri wa Fedha, lakini pia Wizara ya Mambo ya Nje ni lazima tuwe na Waziri wa kutusemea.
Mwaka huu
wabunge ni ya 350 wanaotoka CCM tofauti na miaka mingine na bado kuna
nafasi kumi za wabunge wa kuteuliwa,hivyo sikutaka niteue haraka
haraka,amesisitiza Rais Magufuli
Aidha Dk Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ni kiongozi mnyenyekevu, msikivu ambaye amefanya kazi kubwa katika kipindi cha kwanza cha Serikali ya awamu ya tano lakini akamtaka kutokuwa na uhakika wa nafasi yake badala yake amtangulize Mungu huku akichapa kazi kwa bidii.
” Waziri Mkuu nikupongeze sana kwa nafasi hii, nilikuwa naangalia mawaziri wakuu wenzako waliopita muda waliokaa nikaona nikuteue haraka haraka sasa sijui nilipatia? Maana Nyerere alikaa mwaka mmoja, Kawawa mitatu, Sokoine mitatu, Msuya mitano, Sokoine akarudi akakaa mwaka mmoja tena, Dk Salim akakaa mwaka mmoja, Wariona mitano, Malecela minne na Msuya akarudi kukaa mmoja, Sumaye yeye ndio alikaa miaka 10 yote, Lowassa mitatu na Pinda saba.
Hivyo ndugu zangu nataka muelewe kuwa nafasi ya uwaziri mkuu siyo ya ‘guarantee’ sana itategemea na ufanyaji kazi wake hivyo umuombe sana Mungu na wabunge pia mumuombee ili aweze kufikia rekodi ya Sumaye na Mama Majaliwa pia uelewe una kazi ya kumuombea mumeo,” Amesema Dk Magufuli.
Wasaidizi wangu waliniletea ushauri niteue Waziri wa Mambo ya Ndani na wa Ulinzi sikuwajibu, nikanyamaza kwa sababu sikuona ulazima wa kufanya hivyo haraka, Mkuu wa Majeshi hata akiwa na shida hatoenda kwa Waziri atakuja kwangu, hivyo hivyo kwa IGP na Makatibu Wakuu wapo hivyo tuna haja ya kusubiri na wala hakuna haraka ya kuchagua baraza,” Amesema Rais Magufuli.
Aidha Dkt.Magufuli amewataka wabunge kuondoa presha walizonazo za uchaguzi na kuacha kwenda kwa waganga kuloga kwani watajitia nuksi na badala yake wajikite katika kazi ya kuwatumikia wananchi wao waliowachagua kwani ndio kazi waliyoiomba na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya utekelezaji wake.