RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, hafla hiyo inayofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma.(Picha na Ikulu)