Mchezaji huyo alibuka na Ushindi Baada ya kupiga Mikwaju 147 akifuatiwa na Vicent Gulo wa TPC aliyefungana na Isihaka Daudi wa Lugalo ambaye ameshika nafasi ya Tatu kwa Mikwaju 149.
Kwa Upande wa Divisheni A Mshindi ni Nahuum Gabriel aliyepata Mikwaju ya Jumla 147 akifuatiwa na Juma Mcharo aliyepiga Mikwaju ya Jumla 148.
Kwa Upande wa Divisheni B Mshindi ni Private Laurent Sangawe aliyepiga Mikwaju ya Jumla 149 akifuatiwa na Private Haridi Shemdolwa wote wa Lugalo Baada ya kupata Mikwaju ya jumla 152.
Divisheni C Mshindi ni Sahif Kanabhai wa Arusha baada kupiga Mikwaju ya Jumla 154 akifuatiwa na Issa Issa wa TPC kwa Mikwaju ya Jumla 147.
Kwa Upande wa Wanawake Mshindi ni Madina Iddi kwa Mikwaju ya jumla 146 akifuatiwa na Neema Ulomi wote hao ni wa Arusha huku kwa wazee Ashik Nanabhai wa Arusha akiibuka mshindi.
Kwa upande wa Watoto Viwanja Tisa Mshindi ni Zacharia George na Viwanja 18 Mshindi ni Ibrahim Gabriel kwa Mikwaju ya Jumla 145.