Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma,Sosthenes Kibwengo,akizungumza kwenye mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo,akizungumza na wanafunzi wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Afisa Elimu na Takwimu Dodoma jiji,akitoa neno fupi wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Mlezi wa Klabu ya wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Umonga Mwl John Chakupewa akizungumza wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Mkuu wa shule ya Sekondari Umonga Leticia Singo,akitoa neno la utambulisho wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Baadhi wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma wakionyesha onyesho la Ukakamavu.
Baadhi ya wanafunzi wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma, Sosthenes Kibwengo,(hayupo pichani) wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma, Sosthenes Kibwengo,ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma akigawa Vyeti kwa wahitimu hao.
Mwalimu Mlezi TAKUKURU klabu ya Chinangali Sekondari akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma, Sosthenes Kibwengo,wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma, Sosthenes Kibwengo akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhudhuria mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wanachama wa klabu za wapinga Rushwa kwa shule nane zilizopo jijini Dodoma.
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma,Sosthenes Kibwengo amewataka wahitimu wa kidato cha nne waliopo katika klabu za kupinga rushwa jijini hapa kwenda kuwa mabalozi wa harakati za kupinga rushwa ya ngono katika maeneo wanayoishi.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma wakati wa mahafali ya wahitimu hao iliyojumuisha shule nane za Sekondari
Kibwengo amewataka wahitimu hao wanapokuwa uraiani kusaidia kutoa taarifa pale wanapoona kuna vitendo vya rushwa ya ngono ili taasisi hiyo izifanyie kazi taarifa.
“ Uwezo wa kupambana na rushwa waliuonyesha wakati wakiwa shuleni wakauonyeshe pia uraiani, kwa sababu baadhi ya jamii wamekuwa wakificha taarifa za rushwa ya ngono na rushwa nyingine na kupelekea ugumu wa taasisi hiyo kumkamata muhusika wa kitendo hiko”, ameeleza Kibwengu
Aidha amesema wao kama mabalozi wanapaswa kuongea,kukemea,kuelimisha na kutoa taarifa juu ya suala zima la rushwa.
Naye Afisa elimu vifaa na Takwimu Dodoma Vijijini Fredrick Mwakisambwe niaba ya Afisa Elimu wa shule za sekondari amesema Jumla ya wanafunzi 341 ambao ni wanachama wa klabu nane za kupinga rushwa za shule ya sekondari wanatarajia kuhitimu masomo ya kidato cha nne.
Mwakisambwe ameeleza kuwa mafunzo waliopatiwa niya namna ya kupambana na rushwa kutoka kwa Takukuru na walimu walezi wa klabu hizo wakayatumie wakiwa uraiani kuwaelimisha wasio jua haki zao za msingi juu ya kupambana na rushwa.
“hakuna sababu ya wao kurudi nyuma na harakati za kupambana na rushwa kama walivyofundishwa kupitia klabu za kupinga rushwa wakiwa shuleni isipokuwa mkawe mstari wa mbele kuongoza mapambano ya rushwa”, amesisitiza Mwakisambwe.
Pia ameongeza kuwa ya ngono na rushwa nyingine ipo katika jamii yetu,hivyo bila taarifa kutoka kwenu nyie ambao tayari mmeshakuwa mabalozi wa kupinga rushwa hapa jijini na sehemu nyingine,chombo husika akiwezi kufanya chochote.
Hata hivyo amesema kuwa umoja mliouonyesha kwenye mahafali ya kwanza ya klabu za kupinga rushwa mkauonyeshe pia mkiwa uraiani na kuongeza kuwa wanahitaji kuona elimu ya rushwa ya ngono walioipata wakiwa shuleni kutoka kwa maafisa Takukuru na walimu walezi wanaipeleka pia uraiani.