Na John Walter-Manyara
Rais Dr. John Pombe Magufuli leo Novemba 12,2020 akihutubia wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 Jijini Dodoma, amesema katika kipindi cha miaka mitano katika usafiri wa anga, kutajengwa kiwanja Kikubwa kipya cha Msalato, kufanya upanuzi na ukarabati wa Viwanja kumi na moja (11) vikiwemo vya Kigoma, Shinyanga,Sumbawanga, Tabora, Mtwara, Songea.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa kutajengwa viwanja vya kutua na kuruka ndege kwa kiwango cha lami kwenye Viwanja vya Iringa, Lake Manyara, Tanga, Musoma, Lindi, Kilwa Masoko, Njombe,Singida,Simiyu na kadhalika.
Mbali na hayo, Rais Dr. John Pombe Magufuli amesema atanunua Ndege mpya tano, moja ikiwa ni ya mizigo.
Mbali na hayo, Rais Dr. John Pombe Magufuli amesema atanunua Ndege mpya tano, moja ikiwa ni ya mizigo.
Aidha Dr. Magufuli amesema kuwa Mwaka huu wametunga sheria mpya ya kusimamia na kuendeleza uvuvi wa bahari kuu ambapo wamepanga kununua meli nane za uvuvi kwa kushirikiana na shirika la IFAD, meli hizo nane, Nne zitakuwa upande wa Zanzibar na Nne zitakuwa upande wa Tanzania Bara ambazo meli hizo zitashiriki katika uvuvi wa bahari kuu huku wakikusudia kujenga bandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira elfu 30.
Katika Dr. Magufuli amesema ili kuvutia Uwekezaji, kwenye Sekta ya viwanda wataendelea kuboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji ikiwemo kuangalia masuala ya kodi na kuondoa vikwazo na urasimu ambapo kumekuwepo na Urasimu mwingi na kusumbuliwa kwa wawekezaji kwa kuzungushwa hali inayowafanya wakate tamaa.
Amesema anataka mwekezaji mwenye fedha akija apate kibali ndani ya muda wa siku kumi na nne (14), na kwa sababu hiyo ameamua suala la uwekezaji ikiwa ni pamoja na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kulihamishia kutoka ofisi ya waziri mkuu kwenda ofisi ya Rais ili wanaokwamisha akapambane nao yeye mwenyewe.
Rais John Pombe Magufuli anaendelea kuongoza nchi ya Tanzania katika awamu ya pili na ya mwisho ambapo awali aliingia madarakani mwaka 2015 akiwa na kaumbi mbiu “HAPA KAZI TU” na sasa mwaka 2020-2025 akiongozwa na Kauli mbiu ya “ACHA KAZI IENDELEE”