RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa Dini ya Kiislam Jijini Dodoma baada ya kumaliza kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Nunge Dodoma leo 6-11-2020, na kuwanasihi kuendeleza Amani Nchini
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa Sheikh Abdi Mussa, baada ya kumaliza kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika leo 6/11/2020 katika Masjid Nunge Jijini Dodoma na (kulia kwa Rais) Sheikh. Mohammed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwenyekiti wa Masjid Nunge Dodoma Sheikh.Haji Ismai Abdalla baada ya kumaliza Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Nunge Jijini Dodoma leo 6/11/2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Adam Malima, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Nunge Jijini Dodma leo 6/11/2020.(Picha na Ikulu)
………………………………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini wa dini ya kiislamu nchini kulinda Amani iliyopo ili viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wakatekeleze majukumu yao kwa kuletea maendeleo.
Dkt. Mwinyi ameeleza haya leo Jijini Dodoma baada ya swala ya Ijumaa alipopata nafasi ya kusalimia waumini katika Msikiti wa Nunge.
Aidha Mwinyi amesema kuwa kila mtanzania anawajibu wa kuhakikisha analinda Amani iliyopo ili taifa na wananchi wake kuendelea na shughuli za kimaendeleo.
“Tudumishe Amani yetu, kwani binadamu hathamini kitu mpaka pale kimepotea, hivyo swala la Amani katika taifa letu halina majaribio kwani Amani ikivunjika hatutaweza kupata ibada ya pamoja”,amesisitiza Dkt. Mwinyi.
Vile vile Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa viongozi wa dini zote nchini, wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuliombea taifa kudumisha Amani na kuendelea na shughuli zao za utafutaji.