Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapishwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za Uapisho wake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea eneo la heshma ya kupigiwa Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma leo tarehe 05 Novemba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma leo tarehe 05 Novemba 2020 kwa ajili ya Sherehe za Uapisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kabla ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano katika Muhula wa pili katika sherehe zilizofanyika leo tarehe 05 Novemba 2020 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo akiwa ameshika Mkuki na Ngao mara baada ya kukabidhiwa na Wazee kama ishara ya Kukabidhiwa Madaraka na Ulinzi muda mfupi baada ya kuapishwa leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kuapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU
*********************************************
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa watanzania kuendelea kulijenga taifa na kuacha kuwa taifa tegemezi.
Rais Magufuli ametoa wito huo leo Jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Tano kuongoza kipindi cha pili 2020/2025.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kiapo walichoapa yeye na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ni ishara ya kuanza rasmi kutekeleza miradi na kukamilisha miradi iliyopo, kuondoa umaskini, kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania, kupambana na rushwa na kuendeleza utendaji bora katika watumishi kuwatumikia watanzania.
“Kiapo hiki tulicho apa leo mbele ya Watanzania ni dhamana kubwa kwetu kuhakikisha tunawatumikia na kuwaongoza katika kuleta maendeleo ya taifa hili na kuacha kuwa wategemezi”,amesisitiza Dkt. Magufuli.
Rais Magufuli amesema kujenga uwanja mkubwa wa michezo jijini Dodoma ili kuweza kutosha Watanzania pale watakapo kuwa na shughuli ya kitaifa.
“leo uwanja huu umejaa mpaka watu wengine wako nje na Dodoma ni makao makuu ya Tanzania hivyo kutakuwa na shughuli nyingi za kitaifa ambazo watanzania na wageni mbali mbali watakuwa wanakuja katika hafla hizo”ameeleza Rais Magufuli.
Katika hafla hiyo imeudhuliwa na viongozi mbali mbali wa mataifa mengine ikiwa ni ishara tosha ya ushirikiano mzuri ulipo baina ya Tanzania na mataifa hayo.