Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiapa kuwa Rais wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za Uapisho wake kuwa Rais wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu Tano zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa ameshika Mkuki na Ngao mara baada ya kukabidhiwa na Wazee kama ishara ya Kukabidhiwa Madaraka na Ulinzi muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na Wageni Mbalimbali mara baada ya
kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika
Awamu ya tano katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa akitoa salamu za Wananchi wa
Zimbabwe katika sherehe za Uapisho wa Rais wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe
zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza katika sherehe za Uapisho
wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe za Uapisho wa Rais wa
Tanzania Dkt. John Magufuli katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akipongezwa na Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa mara baada ya sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiteta jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi muda
mfupi mara baada ya sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya
kuapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma.
PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Hatimaye Historia imeandikwa! Ndivyo unavyoweza kueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli amekuwa Rais wa kwanza kuapishwa pamoja na Makamu wake Samia Suluhu katika jiji Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Rais Magufuli amewashukuru wananchi wa Dodoma pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.
”Tofauti na mwaka 2015 niliapishwa jijini Dar es Salama,kwenye uwanja wa uhuru lakini leo niapishwa hapa katika uwanja wa Jamhuri Jiji hili zuri la Dodoma ambapo ndipo Makao makuu ya nchi.
Rais Magufuli amesema kuwa atajenga uwanja mkubwa wa michezo jijini Dodoma ili kuweza kutosha watanzania pale watakapokuwa na shughuli ya kitaifa, “leo uwanja huu umejaa mpaka watu wengine wako nje hivyo lazima tujenge uwanja mkubwa ili shughuli nyingine watu wote waweze kuingia”amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kwa sasa Uchaguzi umekwisha hivyo jukumu kubwa lililopo mbele yetu ni kuendeleza jitihada za kujenga na kuleta maendeleo ya Taifa letu.
”Nawahakikishia Watanzania wote bila kujali tofauti zetu, tutashirikiana katika kutekeleza yote tuliyoyaahidi wakati wa kampeni pamoja na kuendelea kulinda na kudumisha amani na usalama wa nchi yetu, Muungano pamoja na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar”ameeleza
Kwa upande wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa natoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kushinda uchaguzi pamoja na watanzania wote kwa ushindi uliotawaliwa na amani,miezi michache nyuma ilitangazwa Tanzania imeingia kwenye Uchumi wa Kati, mmetuwahi kidogo lakini na sisi tunakuja.
“Baada ya Uhuru Viongozi waligawanyika, wengi walichukua mstari wa kuwa Vibaraka wa Nje, wachache waliipigania Afrika akiwemo Mzee Nyerere, Kaunda, Nkrumah na wengine, Hayati Mzee Moi alitukumbusha neno moja la nyayo akimaanisha alifuata nyayo kisiasa za Mzee Kenyatta”amesema Rais Museveni
Hata hivyo Rais Museveni ametoa pongezi kwa Tanzania kwa kutangazwa kuingia uchumi wa kati, na sisi Uganda tuko nyuma yenu.