Kampuni kinara ya simu za mkononi ya TECNO, imetoa ofa ya zawadi kwa wateja wake wa kwanza kabisa watakaofanya malipo mapema yaani ku Pre-order simu yake mpya kabisa ya TECNO CAMON 16s ambayo inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.
Katika ufafanuzi wake kwenye taarifa ya mpango kazi wa promosheni hiyo ni kwamba mteja atakaye pre-order kwenye maduka yaliyoteuliwa atajinyakulia zawadi za papo kwa hapo zikiwemo TECNO power bank na Wireless Speaker.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba promosheni hiyo inaanza rasmi tarehe 3 Novemba 2020 na itadumu kwa muda wa siku saba yaani wiki moja mpaka tarehe 10 Novemba 2020. Katika kipindi hiki cha wiki moja mteja atatakiwa kutembelea maduka yaliyochaguliwa kufanya promosheni hiyo na kuweka oda ya mapema yaani ku Pre-order.
Simu hiyo ya TECNO CAMON 16s ni simu Bab kubwa ya karne yenye kamera nne nyuma huku kamera yake kuu ikiwa ni ang’avu yenye MP48, Screen kubwa ya inch 6.6 na Storage ya GB 128 ROM + GB4 RAM.
Kufuatia ujio wa simu hii mpya, kampuni ya TECNO imechagua takribani maduka 35 nchini, kufanya promosheni ya Pre-oder kama yalivyoorodheshwa odheshwa hapo chini kwenye jedwali pamoja na namba za kuwasiliana moja kwa moja na wahusika.
Pia mteja anaweza ku-Pre-order kwa kutumia link hii: https://cutt.ly/LgPgzVS
Pia unaweza kupata taarifa zaidi kupitia link hii; https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/