Na Mwandishi Wetu, Misungwi
Mabingwa wa kihstoria Tanzania bara Timu ya Yanga SC imeshindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Gwambina FC Uwanja wa Gwambina, wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha jumla ya pointi 23,huku Azam ikiwa na nafasi ya pili kwa Pointi 22 huku kila timu ikicheza mechi tisa.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Biashara United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.

Kwa sare hiyo, Biashara United wamefikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi 10, wakiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi, wakati KMC inabaki nafasi ya tano ikifikisha pointi 15 za mechi 10.
Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea kesho kwa mechi tatu, Simba SC na Kagera Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Namungo FC na JKT Tanzania Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Pwani na Mwadui FC na Ruvu Shooting Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Kikosi cha Gwambina kilikuwa; Ibrahim Isihaka, Revocatus Richard, Amos Kadikilo, Salum Kipaga, Baraka Mtui, Novaty Lufunga, Meshack Mwamita, Yussuf Kagoma, Jimson Mwanure/Rajabu Rashid dk90, Jacob Massawe na Rajab Athumani.
Yanga SC; Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’/Farid Mussa dk76, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Juma ‘Makapu’, Zawadi Mauya, Abdulaziz Makame, Tuisila Kisinda, Waziri Junior/Michael Sarpong dk58, Yacouba Sogne/Ditram Nchimbi dk76 na Deus Kaseke.