NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limewatahadarisha watu watakaoshiriki maandamano wakidai kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kuwa wasituhubutu kwani sheria itachukua mkondo wake.
Tahadhari hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya kuwepo kwa taarifa za maandamano yasiyokoma nchi nzima baada ya vyama viwili vya siasa kudai kutoridhwa na matokeo ya uchaguzi mkuu yalitotangazwa na NEC.
Amesema hali ya usalama kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28,2020 , mkoani Mwanza hali usalama imeendelea kuimarika kwa kiwango cha juu lakini baadhi ya vyama vya siasa, CHADEMA na ACT Wazalendo, vinadai kutoridhishwa na matokeo ya Rais, Wabunge na Madiwani na hivyo kuhamasisha watu kufanya maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima.
“Hata hivyo baada ya kutangazwa matokeo rasmi ya Rais,Wabunge na Madiwani,baadhi vya vyama vya siasa kama CHADEMA na ACT Wazalendo kudai kutoridhika na matokeo yaliyotangazwa na kuanza kuhamasisha watu wafanye maandamano yanayodaiwa kutokuwa na kikomo,”amesema Muliro.
Amesema maandamano hayo haramu yanayohamasishwa, kuitishwa na kuratibiwa na vyama hivyo viwili vya siasa ni kinyume cha sheria za nchi, jeshi la polisi linaiona mipango hiyo inalengo la kuvuruga amani na kuwataka wananchi wasishiriki.
Muliro ameonya kuwa wananchi watakaoandamana watakamatwa wakiwemo viongozi wa vyama wanaoyaratibu na kuhamasisha maandamano hayo watakamatwa na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria badala yake kama wana malalamiko wafuate taratibu na sheria za uchaguzi zilizopo.
Amesema jeshi la polisi halitakubali na ni marufuku mtu ama kikundi chochote kuendelea kuhamasisha na kuratibu maandamano hayo na kuzuia watu wengine kupata haki ya kufanya shughuli zao za kiuchumi, maendeleo,kisiasa na kijamii eti tu sababu ya watu wako barabarani wakipinga matokeo ya uchaguzi.
Aidha Muliro alisema kuwa jeshi la polisi limevumilia kwa kejeli na dhihaka kwa muda mrefu lakini sasa limefikia kikomo na wanaodhani ni mzaha waacheni waingie barabarani watakiona cha moto.
Amesema kuwa limechoka kuvimilia dhahaka na kejeli dhidi yao zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini na kwamba sasa limefika mwisho wa uvumilivu.
Kamanda huyo wa polisi amesema wananchi wamechoshwa na taarifa za kutishwa na kujengewa hofu na vyama pamoja na viongozi wanaochoona vichwani mwao kuwa ndio sahihi kwa sababu tu kundi ama chama fulani ndio chenye haki ya kuzungumza na kuandamana.
“Narudia tena na kutamka rasmi kuwa maandamano hayo yanayohamasishwa na kuratibiwa ni kinyume cha sheria za nchi, wananchi, wazee, wanawake na vijana, wasituhubutu kushiriki kwani wataingia kwenye msuaguano na polisi na hatutakuwa na cha mswalie Mtume,”alisema Muliro.
Amesistiza jeshi hilo halitamvumulia mtu, kikundi ama chama chochote cha siasa kinachopanga, kuratibu ama kushiriki maandamano hayo ambayo yamepingwa marufuku,hatua kali za kisheria zitachukiliwa kwa watakaokaidi.
Ameeleza kuwa tangu kipindi cha kampeni hadi uchaguzi Mwanza hakukuwa na bomu limepigwa na hivyo wanaopanga maandamano wasitake kulifikisha huko jeshi la polisi na atakayethubutu,litakabiliana naye kwani ipo mifumo ya kisheria ya kufikisha malalamiko ya uchaguzi mahakamani.sssss
POLISI YAONYA MAANDAMANO YASIYOKOMA MWANZA
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza limewatahadarisha watu watakaoshiriki maandamano wakidai kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kuwa wasituhubutu kwani sheria itachukua mkondo wake.
Tahadhari hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ya kuwepo kwa taarifa za maandamano yasiyokoma nchi nzima baada ya vyama viwili vya siasa kudai kutoridhwa na matokeo ya uchaguzi mkuu yalitotangazwa na NEC.
Amesema hali ya usalama kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28,2020 , mkoani Mwanza hali usalama imeendelea kuimarika kwa kiwango cha juu lakini baadhi ya vyama vya siasa, CHADEMA na ACT Wazalendo, vinadai kutoridhishwa na matokeo ya Rais, Wabunge na Madiwani na hivyo kuhamasisha watu kufanya maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima.
“Hata hivyo baada ya kutangazwa matokeo rasmi ya Rais,Wabunge na Madiwani,baadhi vya vyama vya siasa kama CHADEMA na ACT Wazalendo kudai kutoridhika na matokeo yaliyotangazwa na kuanza kuhamasisha watu wafanye maandamano yanayodaiwa kutokuwa na kikomo,”amesema Muliro.
Amesema maandamano hayo haramu yanayohamasishwa, kuitishwa na kuratibiwa na vyama hivyo viwili vya siasa ni kinyume cha sheria za nchi, jeshi la polisi linaiona mipango hiyo inalengo la kuvuruga amani na kuwataka wananchi wasishiriki.
Muliro ameonya kuwa wananchi watakaoandamana watakamatwa wakiwemo viongozi wa vyama wanaoyaratibu na kuhamasisha maandamano hayo watakamatwa na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria badala yake kama wana malalamiko wafuate taratibu na sheria za uchaguzi zilizopo.
Amesema jeshi la polisi halitakubali na ni marufuku mtu ama kikundi chochote kuendelea kuhamasisha na kuratibu maandamano hayo na kuzuia watu wengine kupata haki ya kufanya shughuli zao za kiuchumi, maendeleo,kisiasa na kijamii eti tu sababu ya watu wako barabarani wakipinga matokeo ya uchaguzi.
Aidha Muliro alisema kuwa jeshi la polisi limevumilia kwa kejeli na dhihaka kwa muda mrefu lakini sasa limefikia kikomo na wanaodhani ni mzaha waacheni waingie barabarani watakiona cha moto.
Amesema kuwa polisi wamechoka kuvumilia dhihaka na kejeli dhidi yao zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini na kwamba uvumilivu huo sasa umefika mwisho.
Kamanda huyo wa polisi amesema wananchi wamechoshwa na taarifa za kutishwa na kujengewa hofu na vyama pamoja na viongozi wanaochoona vichwani mwao kuwa ndio sahihi kwa sababu tu kundi ama chama fulani ndio chenye haki ya kuzungumza na kuandamana.
“Narudia tena na kutamka rasmi kuwa maandamano hayo yanayohamasishwa na kuratibiwa ni kinyume cha sheria za nchi, wananchi, wazee, wanawake na vijana, wasituhubutu kushiriki kwani wataingia kwenye msuaguano na polisi na hatutakuwa na cha mswalie Mtume,”alisema Muliro.
Amesistiza jeshi hilo halitamvumulia mtu, kikundi ama chama chochote cha siasa kinachopanga, kuratibu ama kushiriki maandamano hayo ambayo yamepingwa marufuku,hatua kali za kisheria zitachukiliwa kwa watakaokaidi.
Ameeleza kuwa tangu kipindi cha kampeni hadi uchaguzi Mwanza hakukuwa na bomu limepigwa na hivyo wanaopanga maandamano wasitake kulifikisha huko jeshi la polisi na atakayethubutu, litakabiliana naye kwani ipo mifumo ya kisheria ya kufikisha malalamiko ya uchaguzi mahakamani