Muliro alitoa kauli hiyo jan wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi mkuu uliofnyika Oktoba 28, mwaka huu.
Alisema katika Mkoa wa Mwanza,jeshi l polisi liliimarisha usalama kwa kiwango cha juu na kuufanya uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kufanyika kwa haki, uhuru,amani na utulivu bila bughudha.
“Jeshi la polisi linawapongeza wadau wa uchaguzi ambo walitoa taarifa mbalimbali za watu waliokuwa wakipanga njama za kufanya vurugu na fujo ambo walikamatwa na kuhojiwa baadaye kuachiwa kwa dhamana na kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani,hakuna matukio makubwa ya ajabu ya kuathiri mchakato wa uchaguzi mkuu,”alisema Muliro.
Alisema jeshi hilo linafuatilia kwa karibu mchakato wote wa uchaguzi mkuu 2020, kabla, wakati na baada ya kupiga kura katika wilaya na majimbo yote na zipo taarifa za vikundi ama watu kupanga kufanya vurugu.
Muliro alisema wanaendelea kufuatilia mienendo ya taarifa za watu wanaodaiwa bado wana mipango ya kutaka kufanya fujo au vitendo vya kihalifu.
Alieleza kuwa jeshi hilo halitamvumilia mtu yeyote ama kikundi chochote kitakachobainika kuandaa mipango ya kufanya vitendo vyovyte vinavyokinzana na sheria za nchi.
“Polisi hawataruhusu kundi la watu kula njama za kufanya fujo baada ya matokeo yote ya uchaguzi kutangazwa, watakaothubutu watajiingiza kwenye mgogoro na msuguano na jeshi la polisi, hatutakubali watu kuingia barabarani na hatutamvumilia yeyote na atakayethubutu kupanga njama hizo za vurugu,”alisema Muliro.